Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumamosi: Real Madrid wanafanya mazungumzo kuhusu kumrudisha José Mourinho
Real Madrid wako katika mazungumzo na wakala wa José Mourinho kuhusu uwezekano wa kumteua kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo. Mourinho, ambaye kwa sasa anaifundisha SL Benfica, anadaiwa kutaka udhibiti kamili wa timu na ushawishi mkubwa katika masuala ya usajili. (Athletic - subscription required)
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea FC na Manchester United ameripotiwa kuwasiliana moja kwa moja na Real Madrid. (Sky Germany)
Newcastle United na Chelsea FC wanamfuatilia mshambuliaji Darwin Núñez, ambaye anaweza kuondoka Al-Hilal SFC. (Daily Star)
Vilabu kadhaa vikubwa Ulaya, Arsenal FC, Liverpool FC, FC Bayern Munich na FC Barcelona, vinamvizia winga Bradley Barcola wa Paris Saint-Germain. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Atlético Madrid wako karibu kukamilisha dili la kumsajili kiungo João Gomes kutoka Wolverhampton Wanderers kwa takriban pauni milioni 39.(Givemesport)
Inter Milan wanazingatia kuachana na mpango wa kumsajili mlinda lango Guglielmo Vicario wa Tottenham Hotspur ili kuimarisha maeneo mengine ya kikosi chao.(Corriere dello Sport - in Italian)
Leeds United bado wanaonekana kuwa wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji Lois Openda wa Juventus FC, licha ya ushindani kutoka Coventry City. (Football Insider)
Newcastle United pia wanapanga kubadilisha mfumo wao wa usajili na kuajiri skauti wapya katika maeneo mapya kama Balkan, huku Shola Ameobi akitarajiwa kuondoka katika nafasi yake ya usimamizi wa wachezaji wa mkopo. (The i)