Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Waziri Mkuu Starmer akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu, huku Labour ikipoteza kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi

Sir Keir Starmer amesisitiza kuwa hatajiuzulu kama waziri mkuu na “kuitumbukiza nchi kwenye vurugu,” wakati chama cha Labour kikikabiliwa na hasara kubwa katika uchaguzi.

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Donald Trump amesema kuwa Urusi na Ukraine zitasitisha mapigano kwa siku tatu

    Donald Trump ametangaza usitishaji wa mapigano wa siku tatu kati ya Urusi na Ukraine, baada ya nchi hizo mbili kushutumiana kwa kukiuka usitishaji wa mapigano uliotangazwa na kila upande kwa ajili ya maadhimisho ya ushindi wa Umoja wa Kisovieti dhidi ya Ujerumani ya Nazi.

    “Usitishaji huu wa mapigano utahusisha kusimamishwa kwa shughuli zote za kivita, pamoja na kubadilishana wafungwa 1,000 kutoka kila nchi,” rais huyo wa Marekani alisema.

    Muda mfupi baadaye, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alithibitisha ushiriki wa Ukraine katika makubaliano hayo, huku vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vikisema kuwa Urusi pia imekubali pendekezo hilo.

    Awali, pande zote mbili zilidai kuwa upande mwingine uliendelea kushambulia maeneo yao, na meya wa Moscow alisema mji huo ulikuwa umelengwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani usiku kucha.

    Katika ujumbe wake, Trump alisema aliomba binafsi usitishaji huo wa mapigano wa siku tatu na “anathamini sana kukubaliwa kwake na Rais Vladimir Putin pamoja na Rais Volodymyr Zelenskyy.”

    Putin alikuwa ametangaza usitishaji wa mapigano kwa tarehe 8 hadi 9 Mei kabla ya maadhimisho ya Siku ya Ushindi yaliyopangwa kufanyika Jumamosi. Kyiv hapo awali ilikuwa imetoa wito wa usitishaji wa mapigano usio na kikomo kuanzia tarehe 6 Mei.

    Urusi imeionya Ukraine kutofanya jaribio lolote la kushambulia gwaride la Siku ya Ushindi litakalofanyika katika Red Square mjini Moscow.

    Wizara ya ulinzi ya Urusi imetishia kufanya “shambulio kubwa la kulipiza kisasi kwa makombora” katikati mwa mji wa Kyiv ikiwa Moscow itashambuliwa. Pia imewaonya wanadiplomasia wa kigeni kuondoka katika mji mkuu wa Ukraine kabla ya tarehe 9 Mei.

    Unaweza kusoma;

  2. Iran yaishutumu Marekani kwa “hatua za kijeshi zisizo na tahadhari”

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameishutumu Marekani kwa kuchagua “hatua za kijeshi zisizo na tahadhari” kila mara “suluhisho la kidiplomasia linapowekwa mezani.”

    Katika ujumbe aliouchapisha kwenye X, Araghchi alisema kuwa Wairani “hawatasalimu amri kwa shinikizo,” siku moja baada ya pande zote mbili kushutumiana kwa kufanya mashambulizi katika Mlango Bahari wa Hormuz, huku Marekani ikiendelea kushambulia vyombo zaidi vya Iran.

    “Je, hii ni mbinu ya shinikizo la moja kwa moja?” alihoji mwanadiplomasia huyo wa Iran. “Au ni matokeo ya mtu anayeharibu mambo kumdanganya tena Rais wa Marekani Donald Trump na kumuingiza katika mgogoro mwingine?”

    Licha ya mapigano hayo, Trump alisema kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano bado yanaendelea kuheshimiwa. Makubaliano hayo yanatarajiwa kuwezesha mazungumzo ya kumaliza vita ambavyo Marekani na Israel walivianzisha mwezi Februari.

    Iran ilitarajiwa kujibu mapendekezo ya Marekani siku ya Ijumaa, kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio.

    “Natumaini ni pendekezo la dhati, kweli natumaini hivyo,” Rubio alisema akiwa katika ziara nchini Italia.

    Iran imekuwa ikidhibiti Mlango bahari wa Hormuz pamoja na kushambulia washirika wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi kama kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Marekani na Israel.

    Takribani asilimia 20 ya mafuta na gesi asilia duniani hupitia katika njia hiyo muhimu ya maji, na kuzuiwa kwake kumesababisha bei kupanda kwa kasi.

    Mapema wiki hii, Trump alianzisha, kisha kusitisha operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyolenga kusaidia kuachilia zaidi ya meli 2,000 ambazo zimekwama katika eneo hilo tangu Februari.

    Unaweza kusoma;

  3. Waziri Mkuu Starmer akabiliwa na shinikizo la kujiuzulu, huku Labour ikipoteza kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer amesisitiza kuwa hatajiuzulu na “kuitumbukiza nchi kwenye mgogoro,” wakati chama cha Labour kikikabiliwa na hasara kubwa katika uchaguzi.

    Matokeo ya uchaguzi nchini England, Scotland na Wales yameongeza shinikizo kwa Sir Keir, huku baadhi ya wabunge wa Labour wakimtaka kuweka ratiba ya kuondoka kwake madarakani, ingawa kwa sasa washirika wake wa baraza la mawaziri wanaendelea kumuunga mkono.

    Labour imepoteza madaraka nchini Wales, na hivyo kumaliza utawala wake wa miaka 27, huku chama cha SNP kikiendelea kuwa chama kikubwa zaidi nchini Scotland.

    Chama cha Reform UK ndicho kilichopata mafanikio makubwa zaidi nchini England, kikitwaa zaidi ya viti 1,400 na kuchukua udhibiti katika maeneo ambayo kihistoria yalitawaliwa na Labour na Conservatives.

    Chama cha Labour kimepoteza zaidi ya viti 1,100 vya halmashauri nchini England, ikiwemo katika ngome zake za kisiasa kaskazini mwa England na maeneo ya Midlands, na kinatarajiwa kukumbana na matokeo mengine magumu.

  4. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu za leo