Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Njia tatu za kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ubongo
Ubongo wetu unastawi katika mazingira yenye changamoto; hata hivyo, si kila kitu kinapaswa kuwa kazi ngumu ili kupata manufaa ya afya.
Hizi hapa njia tatu rahisi na za kufurahisha za kulinda ubongo wetu tunapozeeka
Ukipewa nafasi ya kufanya kazi mbili- moja rahisi na nyingine ngumu- utachagua kufanya ipi? Kuna uwezekan mkubwa huenda akachagua kufanya kazi rahisi kwa sababu nzuri.
Kuchukua njia za mkato za kiakili ni jambo la kiasili linalotokana na mfumo wetu wa kibiolojia, mkakati wa mageuzi ulioundwa ili kuhifadhi nguvu yetu..
Teknolojia imeongeza uwezo huu tu. Ndio maana tunavutiwa sana kuchukua njia za mkato na kukamilisha kazi kwa msuguano mdogo iwezekanavyo.
Teknolojia imeimarisha uwezo huu tu. Ndio maana tunavutiwa sana kuchukua njia za mkato ili kukamilisha kazi kwa muda mfupi iwezekanavyo.
Lakini, ikiwa hii itasababisha kupungua kwa juhudi za kiakili, inaweza kuathiri maisha yetu na afya kwa ujumla.
Kipindi chetu cha "maisha yenye afya" - yaani, idadi ya miaka ambayo watu hutumia kufurahia afya njema - inapungua katika sehemu nyingi za dunia.
Kulingana na utafiti, kadiri watu wanavyoishi maisha marefu zaidi, idadi ya miaka wanayotumia wakiwa na matatizo ya kiafya huelekea kuongezeka.
Kuhusu ubongo, kuna hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kukuza maisha marefu na yenye afya.
Kimsingi, tunapofanya shughuli zilizo na "changamoto" tunaunda kile kinachojulikana kama "hifadhi ya utambuzi", ambayo ina athari ya kinga kwenye ubongo.
Na kuna njia nyingi za kufanya hivyo katika maisha yetu ya kila siku.
"Haijalishi umri wetu wowote, kuna mambo ambayo tunaweza kufanya - kwa kiwango kikubwa au kidogo - ambayo yanaweza kuongeza uwezo wetu wa utambuzi," anasema mwanasaikolojia Alan Gow, kutoka Chuo Kikuu cha Heriot-Watt huko Edinburgh, Scotland.
Na habari njema ni kwamba hatuhitaji kubadilisha kwa kiasi kikubwa taratibu zetu: kuleta tu mabadiliko madogo, ya taratibu katika nyanja za kimwili, kijamii na kiakili inatosha kulinda ubongo wetu.
Katika taarifa hii tunaangazia njia tatu zenye manufaa zaidi ili kuanza.
1. Kujua uendako bila kutumia ramani
Nji amoja wa kujilinda dhidi ya kupungua kwa utambuzi unaohusiana na umri ni kuzingatia sehemu mahususi ya ubongo.
Hippocampus—eneo la ubongo ambalo ni muhimu kwa urambazaji wa anga—inaaminika kuwa sehemu ya kwanza ya ubongo iliyoathiriwa na ugonjwa wa Alzheimer, miaka kadhaa kabla ya dalili kuanza kuonekana.
"Tumebaini kwa miaka mingi kwamba watu walio na Alzheimer mara nyingi huchanganyikiwa; hii kwa kawaida ni mojawapo ya dalili za awali," anaelezea daktari wa neva Dennis Chan, kutoka Chuo Kikuu cha London (Uingereza), ambaye ni mtaalamu wa kutambua mapema ugonjwa huo.
Na ugunduzi wa mapema ni muhimu, anaongeza: "Kadiri tunavyotambua mapema [upungufu wa utambuzi], ndivyo tunavyoweza kuchukua hatua za haraka."
Kwa hivyo, kulinda eneo hili la ubongo kunaweza kusaidia kuzuia au kuchelewesha mwanzo wa dalili.
Kwa mfano, tafiti kadhaa zinaonyesha kwamba madereva wa ambulensi na teksi wana mojawapo ya viwango vya chini vya vifo vinavyohusishwa na Alzheimer ikilinganishwa na fani nyingine; hii ni kwa sababu, kulingana na watafiti, madereva hawa wametumia akili zao zaidi katika "utambuzi wa mazingira mapya".
Pia imejulikana kwa muda kwamba madereva wa teksi ambao wametumia miaka kadhaa kukariri mpangilio wa barabara za jiji bila kutumia ramani wana uwezo mkubwa wa kiakili.
Tunashauriwa kukuza uwezo kama huo wa madereza wa ambulensi na teksi kupitia kushiriki michezo inayohusisha matukio yanayofanywa yanayojumuisha kusoma ramani na kunyanyua uzani.
Kufikiria jinsi ya kufika unakoenda bila kutumia ramani ya simu ya mkononi kunaweza pia kuwa na manufaa, ikizingatiwa kuwa matumizi ya GPS yamehusishwa kuathirkia kwa kumbukumbu zetu.
Michezo ya video pia inaweza kusaidia ikiwa imeundwa kwa ubora w unaofaa.
Kwa mfano, utafiti mdogo uliofanywa ukihusisha watu wazima waliozeeka ulibaini kuwa wale waliocheza mchezo wa video wa urambazaji wa anga za juu walipata kuboreshwa kwa kumbukumbu zao.
Hata hivyo, ni vyema kutambua kwamba mchezo huu uliundwa mahsusi na watafiti; kwa hivyo, hii haimaanishi kuwa mchezo wetu wa video tuupendao utasaidia kuboresha kumbukumbu zetu.
2. Kutangamana na watu
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa kushiriki katika shughuli za kijamii hutusaidia kuimarisha uwezo wa ubongo kukumbuka vitu.
Kwa mfano, watu walio na umri wa miaka mia moja ambao wanatangamana na watu katika jamii wana afya bora ya ubongo. Wale waliodumisha hali hii wakiwa na umri wa makamo wameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa utambuzi wa jumla katika uzeeni.
Hii pia imethibitishwa na utafiti mkubwa ambao ulibaini kwamba wale ambao walitangamana zidi katika jamii wakiwa na umri wa makamo na wazee waliofanya hivyo walijiepusha na hatari ya kupata magonjwa ya kiakili kwa 30% hadi 50%.
Kulingana na utafiti uliofanywa ukijumuisha wazee 1,923 - na kulenga wale ambao waliishia kupata shida ya akili - wale ambao hawakuwa na muenendo wa kutangamana kijamii walipata ugonjwa wa kiakili miaka mitano mapema kuliko wale ambao walikumbatia hilo.
Inaaminika kuwa kudumisha maisha ya kijamii husaidia kupunguza dhiki, na kutufanya kustahimili changamoto za maisha.
"Uwezo wa kutangamana na jamaa na marafikina kushiriki mazungumzo ya kubadilishana mawazo pia kunaweza kuboresha afya ya akili," anasema Pamela Almeida-Meza, mtaalamu wa magonjwa katika Chuo cha King's College London.
Tunapotangamana na watu wengine, tunasisimua maeneo mengi ya ubongo: kutoka kwa yale yanayohusiana na lugha na kumbukumbu hadi yale yanayohusika katika upangaji wa siku zijazo.
"Kuna kipengele cha utambuzi ambacho huchochea akili. Kwa hiyo, hii inaweza kukuza afya ya ubongo; lakini pia tunajua kwamba kudumisha uhusiano mzuri wa kijamii hupunguza idadi ya matatizo ya kisaikolojia," Gow anasema.
3. Kuendelea kujifunza maishani
Jambo muhimu la kutabiri kwa kuzeeka kwa mafanikio ni idadi ya miaka ambayo mtu hutumia katika elimu.
Wale wanaotumia muda mwingi katika elimu wana hatari ndogo ya kupata shida ya akili.
Mafunzo ya maisha yote yanaweza kuchangia katika kukuza manufaa sawa ya afya ya ulinzi.
Ubongo wetu hustawi kutokana na changamoto na mambo mapya, kwani hii huimarisha maeneo ya ubongo yaliyo hatarini zaidi kwa kuzeeka.
Imeonyeshwa kuwa kuweka ubongo wetu hai hupunguza kasi ya kupungua kwa utambuzi.
Sababu kuu ya jambo hili ni kwamba kujifunza huzalisha neurons mpya na, wakati huo huo, huimarisha zilizopo, ambazo zinaweza kufanya kama utaratibu wa ulinzi dhidi ya kuzeeka na kifo cha seli.
Hii ni neuroplasticity katika hatua: uwezo wa ubongo kujirekebisha na kujigeuza katika maisha yetu yote.
"Ni uwezo huu wa kuzalisha upya seli za neva na sinepsi, ambazo huwapa watu ujasiri dhidi ya Alzheimer" anasema Chan.
Sote tunaweza kuongeza hifadhi yetu ya utambuzi kadri tunavyozeeka.
Katika utafiti wa muda mrefu uliofuata washiriki tangu utotoni hadi mwishoni mwa miaka ya 60, Almeida-Meza na wenzake waligundua kuwa hifadhi ya utambuzi iliongezeka kupitia shughuli za kuimarisha, kama vile elimu na shughuli za burudani.
Wale walioiendeleza walionyesha kupungua kwa kumbukumbu, hata wale waliopata alama za chini kwenye majaribio ya utambuzi wakati wa utoto wao.
Ingawa tunaweza kufaidika katika umri wowote, hili ni muhimu hasa katika hatua za baadaye za maisha, Almeida-Meza adokeza.
Hii ni kwa sababu, tunapozeeka, maisha yetu ya kila siku yanakuwa ya kawaida zaidi na tunapata fursa chache za kujifunza.
Kuna njia mbalimbali za kufikia hili: unaweza kujaribu bustani—ambayo imeonyeshwa kusaidia kuhifadhi utendaji wa utambuzi—, kujiunga na klabu ya vitabu, au kujadili tu kile unachosoma na rafiki.
Hatimaye, kilicho wazi ni kwamba shughuli yoyote inayochangamsha ubongo ni ya manufaa kwa afya kwa ujumla, iwe ni kuchagua njia mpya ya kutembea, kusoma Proust, au kutanguliza mahusiano ya kijamii.