Moja kwa moja, Marekani yaishambulia Iran licha ya makubaliano kuwa karibu kuafikiwa
Majeshi ya Marekani yamesema yamedungua ndege kadhaa zisizo na rubani za Iran zilizokuwa zikielekea katika Mlango bahari wa Hormuz, wakati ambapo Washington na Tehran zimeashiria kuwa karibu kuafikia makubaliano ya kumaliza vita.
Mashambulizi mapya ya Israel yaripotiwa kusini mwa Lebanon
Chanzo cha picha, Getty Images
Vyombo
vya habari nchini Lebanon vimeripoti mashambulizi ya
Israel kusini mwa taifa hilo.
Mashambulizi hayo yametokea baada ya jeshi la Israel kutoa ilani ya watu kuondoka katika zaidi ya maeneo
20 kusini mwa Lebanon, ikiwemo mji wa Nabatieh.
Hapo jana, kundi la Hezbollah lilitangaza kuwa vikosi vyake
vilipigana na wanajeshi wa Israel waliokuwa wakielekea mji wa mpakani kusini mwa
Lebanon.
Mapigano kati ya jeshi
la Israel na Hezbollah yanaendelea,
huku Iran na Marekani zikitangaza kuwa ziko karibu kutia saini makubaliano
ya kumaliza
vita.
Bei ya mafuta yashuka na kufikia viwango vya chini zaidi tangu vita kuanza Iran
Chanzo cha picha, Getty Images
Bei ya mafuta imeshuka na kufikia kiwango cha chini zaidi takriban miezi minne tangu vita vya Iran kuanza.
Kushuka kwa bei hiyo kunatokana na Imani ya
wanabiashara kuwa makubaliano ya kumaliza vita kati ya Iran na Marekani yako
karibu kuafikiwa.
Bei
ya mafuta aina ya Brent imeshuka hadi dola
87.33 kwa pipa moja , ikiwa ni punguzo la dola 3.05 ikiwa kiwango cha chini sana tangu mapema mwezi Machi
vita vilipoanza.
Kwa
upande wa Marekani, mafuta yameshuka kwa dola 2.83 hadi
dola 84.88 kwa pipa moja,
ikiwa ni bei ya chini zaidi ya mafuta hayo tangu mwezi Aprili.
Taarifa za kuashiria kuwa huenda Marekani
na Iran wakakubaliana hivi karibuni imeleta afueni katika soko la nishati
duniani.
Partey anyimwa viza ya Canada, kukosa mechi ya ufunguzi ya Ghana
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa Ghana, Thomas Partey, atakosa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia dhidi ya Panama baada ya kunyimwa kibali cha kuingia nchini Canada. Kwa mujibu wa taarifa, maombi yake ya viza yalikataliwa na serikali ya Canada.
FIFA imethibitisha kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, ambaye kwa sasa anachezea Villarreal, hakuweza kusafiri kutoka kituo cha mazoezi cha Ghana kilichopo Boston kwenda Marekani kutokana na kukosa kibali cha kuingia nchini humo. Shirikisho hilo limesema linaheshimu taratibu za uhamiaji za nchi mwenyeji.
Partey anakabiliwa na kesi ya kujibu mashtaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono, lakini bado hajahukumiwa na amekana mashtaka yote. Hali hiyo imekuwa moja ya sababu zilizoathiri uamuzi wa viza yake.
Serikali ya Canada imesema kila ombi la kuingia nchini linachunguzwa kwa kina kulingana na sheria za uhamiaji na usalama, na kwamba kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia hakubadilishi sheria hizo.
Kocha wa Ghana, Carlos Queiroz, amesema hana mashaka na uteuzi wa mchezaji huyo, akisisitiza kuwa uamuzi wake wa kumjumuisha kikosini ni wa kiufundi na haoni haja ya kuingia kwenye mjadala wa kimaadili kwa sasa.
Ghana inatarajiwa kuendelea na mechi zake za Kundi L bila Partey, huku uwezekano wa mchezaji huyo kurejea baadaye kwenye mashindano ukibaki wazi endapo timu yake itasonga mbele.
Jeshi la Marekani lamuua kiongozi wa genge la Tren de Aragua nchini Venezuela
Chanzo cha picha, Truth Social
Niño Guerrero, ambaye jina lake kamili ni Héctor
Rusthenford Guerrero Flores, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa Tren de
Aragua. Genge hilo ni moja ya makundi hatari
Marekani Kusini na imekuwa ikilengwa na utawala wa Trump.
Rais Trump amelituhumu genge hilo kwa kushiriki katika
“vita visivyo vya kawaida” dhidi ya Marekani na kulitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Rais
Trump alichapisha picha za
video za shambulio hilo la angani, zikionyesha jengo la kijani na kibanda
kilichokuwa karibu kikilipuliwa.
Trump
aliongezea kuwa operesheni
hiyo ya kijeshi ilifanikishwa na
“marafiki wetu nchini Venezuela, ambao tunafanya kazi nao vizuri sana”.
Mamlaka za Venezuela zimethibitisha kushiriki kwao katika kile walichokiita “operesheni ya
pamoja”.
Mwezi
Januari, vikosi vya Marekani
vilimkamata Rais wa wakati huo wa Venezuela Nicolás Maduro na
kumfungulia mashtaka mjini New York, hati ya mashtaka ikimtaja Guerrero Flores kama mshirika wake
katika kutekeleza uhalifu.
Elon Musk ameandika historia kwa kuwa mtu wa kwanza duniani kufikisha utajiri wa zaidi ya dola trilioni moja, baada ya hisa za kampuni yake ya SpaceX kupanda kwa kasi katika siku ya kwanza kuorodheshwa kwenye soko la hisa la Nasdaq.
Kwa mujibu wa orodha ya matajiri ya Bloomberg, utajiri wa Musk umefikia dola trilioni 1.11 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 2,800 za Tanzania), jambo lililomfanya kuimarisha nafasi yake kama mtu tajiri zaidi duniani.
Mafanikio hayo yamechochewa na kuorodheshwa kwa SpaceX katika soko la hisa kwa thamani ya dola trilioni 2.2. Hisa za kampuni hiyo zilianza kuuzwa kwa dola 150 na kufikia dola 176.50 katika muda mfupi kutokana na hamasa kubwa ya wawekezaji.
Musk anamiliki asilimia 42 ya SpaceX, huku thamani ya hisa zake katika kampuni hiyo ikikadiriwa kufikia zaidi ya dola bilioni 767. Pia ana hisa Tesla zenye thamani ya mamia ya mabilioni ya dola.
Marekani yaichapa Paraguay 4-1, kufanya maajabu mwaka huu?
Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani imeanza vyema kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Paraguay mabao 4-1 mjini Los Angeles na kuongoza Kundi D.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Folarin Balogun, alifunga mabao mawili katika ushindi huo mkubwa wa wenyeji wenza wa mashindano hayo.
Katika mchezo mwingine, mwenyeji mwingine Canada ililazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina na kujikusanyia alama moja katika mechi yake ya kwanza ya kundi.
Nayo Mexico ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini, ikiweka wazi dhamira yake ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wake.
Hadi sasa, mataifa yote matatu yanayoandaa Kombe la Dunia 2026 yamecheza mechi zao za ufunguzi, huku Mexico na Marekani zikianza kwa ushindi na Canada ikipata sare. Zitafanya maajabu mwaka huu?
Marekani yamfukuza mwanaharakati wa Iran na kumpeleka Afrika ya Kati
Chanzo cha picha, Reuters
Mwanasheria wa mwanamke mmoja ambaye mwanaharakati wa demokrasia
kutoka Iran amesema kuwa Marekani
imemfukuza mteja wake na kumpeleka katika taifa la Central Africa Republic (CAR), na
kusema ni hatua inayohatarisha maisha ya mteja wake.
Kwa
mujibu wa wakili huyo aliyezungumza na Reuters, Maisha mwanaharakati huyo yapo hatarini kutokana na
vurugu na ukosefu wa amani ambao unashuhudia katika taifa hilo la Afrika ya
Kati.
Taasisi
ya Iranian American Legal Defense Fund iliripoti kuwa wanawake watatu wa Iran
waliokimbia nchi yao walikuwa katika hatari ya kufukuzwa kutoka Marekani.
Abbas Araqchi: Makubaliano ya kumaliza vita na Marekani yako karibu kuafikiwa
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Mambo ya Kigeni
wa Iran, Abbas Araqchi, amesema kuwa makubaliano ya
kumaliza vita kati ya Iran na Marekani yako katika hatua za mwisho, na kwamba Mlango bahari wa Hormuz utafunguliwa tena kama sehemu
ya makubaliano hayo.
Kwa mujibu wa BBC Persian, Araqchi alisema katika mahojiano ya
televisheni kuwa “hatujawahi kuwa karibu hivi na makubaliano kama ilivyo sasa,”
akiongezea kuwa makubaliano hayo yanaweza kuafikiwa ndani ya siku moja au mbili zijazo.
Waziri huyo pia aliviambia
vyombo vya habari nchini Iran kuepuka kutoa taarifa za uvumi ambazo zinaweza kuharibu
mchakato huo wa kidiplomasia na kuathiri mazingira ya mazungumzo.
Araqchi alisema kuwa makubaliano
hayo yana ukurasa mmoja na nusu hadi mbili tu, lakini
yamejadiliwa kwa zaidi ya miezi miwili, ambapo kila kipengele na kila sentensi imepitiwa na kuhaririwa kwa maslahi ya raia wa Iran.
Jeshi la Marekani ladai kudungua ndege zisizo na rubani za Iran katika Mlango bahari wa Hormuz
Chanzo cha picha, US Navy via Getty Images
Kituo kikuu cha kuendesha oparesheni za kijeshi Marekani (CENTCOM) imedai kuwa vikosi vyake vimeangusha ndege kadhaa zisizo na rubani zilizorushwa na Iran kuelekea Mlango bahari wa Hormuz.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema Iran ilirusha ndege zisizo na rubani kadhaa kwa lengo la kulenga meli za kibiashara zilizokuwa zikisafiri kupitia Mlango bahari wa Hormuz.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, "Vikosi vya Marekani vimedungua ndege hizo zote zisizo na rubani katika saa chache zilizopita, na usafiri wa meli kupitia Mlango wa Hormuz unaendelea bila usumbufu wowote."
Centcom ilisema ndege hizo za Iran zilikuwa tishio kwa usalama wa meli za kibiashara zinazopitia eneo hilo.