Mambo matatu ambayo ni kiini cha mzozo wa Trump na Papa Leo XIV

l

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mvutano kati ya Vatican na Ikulu ya White House ulianza miezi kadhaa kabla ya Papa Leo XIII kumtaja Trump moja kwa moja kuhusu vita nchini Iran.
Muda wa kusoma: Dakika 6

Rais wa Marekani Donald Trump na Papa Leo XIV wameingia katika mzozo usio wa kawaida kuhusu vita nchini Iran, baada ya Papa kumtaja Trump moja kwa moja kwa mara ya kwanza.

Alichaguliwa Mei 2025 kama Papa wa kwanza mzaliwa wa Marekani — akiitwa Kardinali Robert Prevost—awali alitumia mtindo wa kutomtaja Trump kwa jina – lakini hilo limebadilika sasa.

Mvutano kati ya Vatican na Ikulu ya White House umekuwa ukiongezeka katika miezi ya hivi karibuni, na kutupiana maneno hivi karibuni kumefichua tofauti hizo.

Sera ya kigeni

l

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Katika mahubiri yake ya Krismasi, Papa Leo XIV alizungumzia "mahema huko Gaza, yaliyo wazi kwa mvua, upepo na baridi."

Mzozo kati ya Trump na Leo XIV ulizidi kuongezeka Jumapili baada ya rais wa Marekani kumshambulia Papa katika chapisho refu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, akisema ni "DHAIFU kupambana na uhalifu, na haelewi sera za kigeni."

"Sitaki Papa anayefikiri ni sawa kwa Iran kuwa na silaha za nyuklia," Trump aliandika.

"Sitaki Papa anayefikiri ni jambo baya Marekani kuishambulia Venezuela, nchi ambayo ilikuwa ikituma kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kwenda Marekani na, mbaya zaidi, imekuwa ikawaachilia wahalifu kutoka magerezani [ili kuwatuma] nchini mwetu, wakiwemo wauaji, wafanyabiashara wa dawa za kulevya, na wahalifu," aliongeza.

Kisha m-Republican huyo alichapisha picha iliyotengenezwa kwa akili bandia ambapo anaonekana mtu kama Yesu anayeonekana "akimponya" mtu, picha iliyosababisha ukosoaji kutoka kwa viongozi wa kidini na wachambuzi.

Kisha picha hiyo ilifutwa.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Papa alikosoa Leo onyo la Trump kwamba Marekani inaweza "kufuta ustaarabu wa Iran" ikiwa Tehran haitatii matakwa katika mazungumzo ya nyuklia na kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz.

Papa alielezea kauli hiyo "halikubaliki kabisa" na akawasihi Wakatoliki kuwashinikiza viongozi wa kisiasa "kufanya kazi kwa ajili ya amani."

Papa Leo alimmtaja Trump moja kwa moja siku zilizopita.

"Nimeambiwa Rais Trump alisema anataka kukomesha vita. Natumai anatafuta suluhisho," aliwaambia waandishi wa habari Machi 31.

Siku ya Jumapili, Papa huyo mwenye umri wa miaka 70 aliwasihi tena viongozi kukomesha umwagaji damu, na kulaani kile alichokielezea kama "udanganyifu wa uwezo wao" unaochochea vita.

Msimamo wa Papa Leo kuhusu Iran ni kama misimamo aliouchukua katika maeneo mengine.

Siku chache tu baada ya kuchaguliwa kwake mwaka jana, alitoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja huko Gaza, kuachiliwa mateka, na kupelekwa kwa mahitaji ya kibinadamu.

Agosti 2025, Papa Leo alilaani kile alichokiita "adhabu ya wote" na kulazimishwa kuhama Wapalestina, na akaelezea hali huko Gaza "haikubalika."

Katika mahubiri yake ya Krismasi, kiongozi wa Wakatoliki bilioni 1.4 duniani alizungumzia "mahema huko Gaza, yanayopigwa na mvua, upepo na baridi."

Ingawa Trump na Papa Leo hawakugombana hadharani kuhusu Gaza wakati huo, wanadiplomasia wa Vatican walielewa kuwa matamshi ya Papa yataleta changamoto kwa Marekani na Israeli.

Na mwezi Januari mwaka huu, Papa alielezea wasiwasi wake baada ya vikosi vya Marekani kumkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro huko Caracas na kumpeleka New York kukabiliwa na kesi.

"Wema wa watu wa Venezuela lazima ushinde mawazo mengine yoyote na kutuongoza kushinda vurugu na kufuata njia za haki na amani," alisema.

Leo XIV pia alihimiza heshima kwa uhuru wa Venezuela, ulinzi wa utawala wa sheria kama ilivyoainishwa katika Katiba, na heshima kwa haki za binadamu na za kiraia.

Uhamiaji

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa amekosoa mara kwa mara sera za uhamiaji za Trump.

Uhamiaji umekuwa chanzo kingine kikubwa cha msuguano.

Papa Leo amekosoa mara kwa mara sera za uhamiaji za Trump, akitaja suala la kuwatendea vyema wahamiaji kuwa ni wajibu wa kimaadili unaotokana na mafundisho ya kiinjili kuhusu huruma na utu.

Novemba 2025, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alisema wageni nchini Marekani wanavunjiwa heshima, akirudia kauli kutoka kwa maaskofu Wakatoliki wa Marekani iliyokosoa kufukuzwa kwa wahamiaji na kuonya kuhusu hofu na wasiwasi unaosababishwa na uvamizi dhidi wahamiaji.

"Naamini tunapaswa kutafuta njia za kuwatendea watu kwa njia za ubinadamu," alisema Papa Leo, huku akikiri kwamba "kila nchi ina haki ya kuamua ni nani, vipi na lini watu wataingia."

Katika hotuba yake katika Uwanja wa St. Peter Oktoba iliyopita, aliwasihi Wakatoliki kutowatendea wahamiaji "vibaya au unyanyapaa na ubaguzi," na baadaye alihoji kama sera za Trump zinaendana na mafundisho ya Kanisa.

Kauli hizo zilisababisha majibu mabaya kutoka kwa Wakatoliki wenye msimamo mkali.

Dini na mamlaka ya kisiasa

l

Chanzo cha picha, TRUTH SOCIAL

Maelezo ya picha, Trump alichapisha—na kisha akafuta—picha iliyotengenezwa na akili bandia iliyomwonyesha mtu anayefanana na Yesu, na kusababisha ukosoaji kutoka kwa viongozi wa kidini na wachambuzi.

Ujumbe wa Trump kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumapili ulikuwa mkali, amemtuhumu Papa Leo XIII kwa kuvuka mipaka yake: "Sitaki Papa anayemkosoa rais wa Marekani kwa sababu ninafanya kile nilichochaguliwa kufanya baada ya ushindi wa kishindo."

Trump alisema Papa alichaguliwa kuwa Papa kwa sababu tu yeye ni Mmarekani, akisema: "Kama nisingekuwa Ikulu ya White House, Leo asingekuwa Vatikani."

Alipoulizwa na waandishi wa habari kuelezea chapisho hilo, baadaye alisema: "Sidhani kama anafanya kazi nzuri. Anapenda uhalifu, nadhani."

"Mimi si shabiki wa Papa Leo," Trump aliongeza, akizungumza kwenye uwanja wa ndege baada ya kurudi Washington kutoka Florida.

Hata hivyo, siku ya Jumatatu, akizungumza ndani ya ndege ya Papa mwanzoni mwa safari ya siku 11 barani Afrika, Leo XIV alikataa kujibizana na Trump.

"Mimi si mwanasiasa na sitaki kuingia kwenye mjadala naye," alisema.

"Nitaendelea kukosoa waziwazi vita, kuhimiza amani, mazungumzo na ushirikiano," Papa aliongeza.

Aliongeza kwamba "haogopi utawala wa Trump" na ataendelea kupaza sauti yake "kwa sauti kubwa" akitetea Injili.

Mgombea huyo wa Republican alishinda 55% ya kura za Wakatoliki katika uchaguzi wa 2024, kulingana na kura ya maoni ya Associated Press.

Wakatoliki wanaunda takriban moja ya tano ya idadi ya watu Marekani, kulingana na Ofisi ya Sensa ya Marekani, akiwemo Makamu wa Rais JD Vance.

Utawala wa Trump pia una uhusiano wa karibu na viongozi wa kiinjili wa Kiprotestanti ambao wametumia maneno ya kidini kuunga mkono vita nchini Iran.

Kadinali Blase Cupich wa Chicago, mshirika wa karibu wa Papa Leo, aliiambia Reuters kwamba Papa anaendeleza utamaduni wa muda mrefu wa Mapapa ambao unawahimiza viongozi wa dunia kuachana na vita.

Marie Dennis, kiongozi wa zamani wa harakati ya kimataifa ya amani ya Kikatoliki, Pax Christi, anasema maoni ya hivi karibuni ya Papa Leo na kumtaja moja kwa moja Trump "yanaonyesha moyo uliovunjika kutokana na vurugu zisizoisha."