Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Chelsea walipewa nafasi ya kumsajili Bissouma
Chelsea walipewa ofa ya kumsajili kiungo wa zamani wa Tottenham na Mali, Yves Bissouma, mwenye umri wa miaka 30, kama mbadala wa Enzo Fernandez, mwenye miaka 25, aliyejiunga na Manchester City kwa pauni milioni 125.(Sun)
Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa klabu zilizokuwa zikimnyemelea kiungo wa England, Adam Wharton, mwenye miaka 22, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Hata hivyo, Crystal Palace ilikataa ofa zote zilizowasilishwa.(Guardian)
Aston Villa, Manchester City na Newcastle United zinaonyesha nia ya kumsajili winga wa Spain, Alex Baena, mwenye miaka 25, lakini Atletico Madrid haina mpango wa kumuuza.(CaughtOffside)
Wolves walikuwa tayari kumuuza mshambuliaji wa timu ya England chini ya miaka 21, Mateus Mane, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Liverpool na Manchester United zilikuwa miongoni mwa klabu zilizomfuatilia kinda huyo mwenye miaka 18.(Teamtalk)
Arsenal inafikiria kutoa ofa ya pauni milioni 68 kumsajili winga wa Barcelona na Brazil, Raphinha, mwenye miaka 29, katika dirisha la Januari.(Fichajes - in Spanish)
Tottenham inafikiria kusitisha mkataba wa Richarlison ili mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye miaka 29, ambaye hapewi nafasi kikosi cha kwanza, aondoke kwa uhamisho wa bure.(Talksport)
Everton ilitoa ofa ya mdomo ya pauni milioni 40 pamoja na bonasi ya pauni milioni tano kwa West Ham kumnunua mshambuliaji wa Argentina, Taty Castellanos. Hata hivyo, ofa hiyo iliwasilishwa muda mfupi kabla ya dirisha kufungwa na West Ham haikuweza kukamilisha uhamisho huo.(Teamtalk)
Newcastle United ilikataa ofa mbili kutoka Nottingham Forest kwa kiungo mshambuliaji wa England, Jacob Murphy, mwenye miaka 31, baada ya kocha Matthias Jaissle kutaka kumuweka kwenye kikosi.(Football Insider)