Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumapili:Juventus kuongeza juhudi kumnasa Silva
Juventus wanapanga kuongeza juhudi kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva, ambaye ataondoka Manchester City msimu huu wa joto, huku wakijaribu kuzipiku Atletico Madrid na Barcelona ili kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Corriere dello Sport)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Deco alitarajiwa katika Fainali ya Kombe la FA kumtazama mshambuliaji wa Chelsea Joao Pedro, licha ya Blues kutotaka kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24. (Mail)
Wachezaji wapya wa Ligi Kuu Coventry City wanafikiria kuhusu mkataba wa kiungo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 35 Georginio Wijnaldum, ambaye mkataba wake na Al-Ettifaq unatarajiwa kuisha msimu huu wa joto. (Football Insider)
Everton wana nia ya kumsajili winga msimu huu wa joto na wanamfuatilia Loum Tchaouna mwenye umri wa miaka 22 wa Burnley, ambaye ameiwakilisha timu ya Ufaransa ya chini ya miaka 21. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Leeds United,Wilfried Gnonto, 22, anatafutwa na klabu ya Ujerumani SC Freiburg na klabu hiyo ya Elland Road iko wazi kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia kuuzwa au kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports Germany)
Mlinzi wa Italia Alessandro Bastoni, 27, amekuwa akihusishwa sana na Barcelona lakini angefurahi kubaki Inter Milan ikiwa uhamisho wake kwenda klabu hiyo ya Hispania hautatimia. (Gazzetta dello Sport )
Juventus inaweza kuamua kumpa kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, ambaye yuko kwa mkopo Aston Villa, nafasi nyingine ya kuvutia isipokuwa waweze kumuuza mchezaji huyo wa miaka 28. (Gazzetta dello Sport)
Bayern Munich ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Atalanta na Ubelgiji Charles De Ketelaere, 25, lakini kama mbadala tu ikiwa uhamisho wa winga wa Uingereza na Newcastle United Anthony Gordon, 25, utashindikana. (Football Italia)