Kombe la Dunia 2026: Canada waidhalilisha Qatar iliyoishia kuwa na wachezaji tisa
Wenyeji Canada wamewadhalilisha wenyeji wa fainali zilizopita za 2022 Qatar kwa kuwachabanga 6-0.
Kila kipindi kilizaa magoli matatu huku Qatar wakimaliza na wachezaji tisa dimbani kutokana na wachezaji wake wawili kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mchezaji Jonathan David wa Canada anayecheza katika klabu ya Juventutus Tulin ya Italia alipachika magoli matatu na kuwa wa pili katika fainali za mwaka huu baada ya Lonel Messi kufanya vivyo hivyo dhidi ya Algeria.
Kabla ya hapo, Uswiss iliionesha Bosnia Herzegovina kile kilichomnyoa kanga manyoya kwa kuwashushia kichapo cha mogili 4-1 huku kiungo Jonathan Manzambi anayesakata soka katika klabu ya Freiburg ya Ujerumani akiziona nyavu mara mbili.
Soma zaidi: