Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Msongo wa mawazo unaofichwa kwa tabasamu' ni nini na unawezaje kuutambua?
Hebu mfikirie mtu mwenye msongo wa mawazo; huenda ukawazia mtu anayepata shida hata ya kuamka kitandani.
Watu wa aina hiyo wanaweza kulia sana, kujitenga na marafiki, au kukosa nguvu kabisa za kumaliza shughuli za siku.
Huenda usingemfikiria mtu anayetoa utani wakati wa chakula cha jioni, mwenye maisha ya kijamii yenye kuchangamka, na anayefanya kazi yake vizuri ofisini.
Lakini hali hii ni ya kawaida kwa watu wanaokabiliwa na hali inayojulikana kama "msongo wa mawazo uliofichwa nyuma ya tabasamu" (smiling depression).
Watu wanaokabiliwa na aina hii ya msongo wa mawazo hujidanganya wenyewe, na si marafiki au wafanyakazi wenzao.
'Unyogovu wa kutabasamu' ni nini?
"Unyogovu uliofichwa nyuma ya tabasamu" (smiling depression) si ugonjwa unaotambulika rasmi, lakini utafutaji wa neno hilo mtandaoni umeongezeka kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
"Inamaanisha kuonekana mwenye furaha kwa nje, ingawa ndani unahisi huzuni na unyogovu," anasema Dkt. Olivia Remes, mtafiti wa afya ya akili katika Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza.
Sote huhisi huzuni wakati fulani. Lakini kulingana na Shirika la Afya Duniani, kwa takriban watu milioni 320 duniani kote, hisia hizo hugeuka na kuwa unyogovu.
Hali hii hutokea wakati dalili kama vile huzuni endelevu au kupoteza hamu na furaha zinapoendelea kwa wiki au miezi, na kuathiri kazi, mahusiano, usingizi, pamoja na maisha ya kila siku.
Hata hivyo, unyogovu haujitokezi kila mara kwa namna tunavyotarajia.
Utafiti unaonyesha kuwa takriban asilimia 40 ya watu wenye unyogovu huhisi "si wa kawaida." Katika hali hizi, dalili hutofautiana na dhana zilizozoeleka.
Kwa mfano, mtu anaweza kulala au kula zaidi badala ya kula au kulala kidogo kuliko kawaida, huku hisia zake zikiimarika kwa muda wakati jambo zuri au la kusisimua linapotokea.
Pia kuna ushahidi unaoonyesha kuwa watu wenye unyogovu hujaribu kuonekana kama watu wengine kwa kuficha dalili au hisia zao jambo linalojulikana kama 'masking' (kujificha nyuma ya sura bandia).
Kwa nini watu huficha hali a msongo wa mawazo ?
Baadhi ya watu wanaokabiliwa na hali inayojulikana kama "smiling depression" (huzuni iliyofichwa nyuma ya tabasamu) hawajui hata kwamba wana huzuni hiyo, hivyo hawafahamu kuwa wanaificha.
"Wanaweza kufikiri kuwa dalili wanazopata ni matokeo ya kawaida tu ya kuishi maisha yenye shughuli nyingi na msongo wa mawazo," anasema Remes.
Baadhi ya watu wanaweza kukiri kuwa wana tatizo, lakini hufanya juhudi kubwa kulificha ili hakuna mtu mwingine atakayeligundua.
"Wanajiwekea viwango vya juu na huenda wasitake kukiri kwao wenyewe au kwa wengine kuwa wana tatizo," anasema Remes.
Watu wengine huogopa unyanyapaa na kuwa mzigo kwa wengine. Utafiti unaonyesha kuwa baadhi ya watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu kukosolewa kazini au katika mahusiano.
Matarajio ya kijamii au ya kifamilia pia yanaweza kuleta vikwazo katika kuzungumzia suala hilo kwa uwazi.
Je, ni hatari gani zinazotokana na kuficha msongo wa mawazo?
Wataalamu wanasema kuwa kujifanya uko sawa (wakati huko hivyo) kunaweza kuwa hatari.
"Unyogovu hututenga na kutufanya tujihisi wapweke, na mara nyingi njia bora ya kushinda huzuni ni kushirikiana na wengine," anasema Profesa Barney Dunn, mwanasaikolojia wa kimatibabu katika Chuo Kikuu cha Exeter, nchini Uingereza.
Hali hiyo pia inaweza kusababisha watu kukosa msaada wanaohitaji.
"Dalili hizi za awali zisiposhughulikiwa, zinaweza kugeuka kuwa matatizo makubwa na ya kudumu, na kuongeza hatari ya kujiua," anasema Remes.
Dalili saba za msongo wa mawazo
Unapokabiliana vyema na hali ya maisha, inaweza kuwa rahisi kupuuza mabadiliko fulani.
1. Unaacha kufurahia mambo
Ikiwa mambo ambayo kwa kawaida unayatarajia kwa hamu – kama vile kukutana na marafiki, kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi, au kutazama kipindi chako pendwa cha televisheni – sasa yanaonekana kuwa mzigo, inaweza kufaa kuchunguza zaidi.
"Ni rahisi kuhusisha ukosefu wa hamu au furaha katika shughuli za kawaida za burudani na mtindo wa maisha wenye shughuli nyingi na kasi kubwa," anasema Remes.
2. Mikono au miguu yako inahisi uzito usio wa kawaida
Hali hii, inayojulikana kama "kupooza kwa Leiden" (Leiden's paralysis), husababisha mikono na miguu kuhisi uzito, na kufanya hata shughuli za kila siku kuhitaji nguvu zaidi. Hii inaweza kuwa ishara ya aina isiyo ya kawaida ya msongo wa mawazo (atypical depression).
3. Unaghairi mipango mara kwa mara
Wakati mwingine unaweza kuonekana kuwa katika hali nzuri kabisa mbele ya wengine, lakini hisia zako zinapoharibika na kushindwa kuzificha, unaghairi mipango yako.
4. Unalala zaidi – lakini bado unahisi uchovu
Unaweza kuwa bado unafanya shughuli zako zote za kawaida, lakini wakati huo huo unahisi uchovu wa kudumu.
"Nyakati za jioni zinaweza kuwa ngumu hasa, kwani watu wenye hali hii wanaweza kuhisi vibaya zaidi mwishoni mwa siku, na wanaweza kuhitaji muda mwingi zaidi wa kulala kuliko kawaida," anasema Remes.
5. Unakuwa na hisia kali zaidi dhidi ya ukosoaji au kukataliwa
Maoni rahisi kutoka kwa bosi wako au rafiki anayehairi mipango yanaweza kukuumiza zaidi kuliko kawaida.
Remes anasema kuwa kuongezeka kwa hisia kali dhidi ya ukosoaji au kukataliwa – hali ambayo pia inaweza kupatikana kwa watu wenye ADHD (tatizo la kutokuwa na umakini na kuwa na uchangamfu kupita kiasi) – ni sifa ya aina isiyo ya kawaida ya msongo wa mawazo.
6. Daima unakuwa mtu wa kuchekesha au mwenye kusaidia
Mtu anayepambana na msongo wa mawazo hajitengi kila wakati na anaweza mara nyingi kuonyesha tabia tofauti kabisa, kama vile kuwa kiini cha furaha kwenye sherehe, kuzama katika kazi, au kujitolea sana kusaidia wengine.
7. Unakuwa na mawazo mabaya kila wakati
Unaweza kuonekana mwenye kujiamini, huku ndani kabisa ukijikosoa sana.
Kutojiamini, kuhisi kutokuwa na thamani, na mawazo ya utupu wa ndani vinaweza kuwa ishara za onyo.