Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Newcastle yafikiria kumuuza Wissa, Delap ataka kubaki Chelsea
Newcastle inatazamiwa kufikiria kumuuza mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa katika dirisha la majira ya kiangazi, chini ya mwaka mmoja tangu imsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kwa ada inayoweza kufikia pauni milioni 55.
Mshambuliaji wa England Liam Delap, 23, anataka kubaki Chelsea na kupigania nafasi yake, huku klabu hiyo ikikabiliwa na maamuzi makubwa kuhusu safu yake ya ushambuliaji.(Telegraph)
Barcelona imeanza mawasiliano na Atletico Madrid ili kufahamu msimamo wa klabu hiyo kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 26, majira haya ya kiangazi. . (ESPN)
Hatma ya Scott Parker kama kocha wa Burnley bado haijulikani baada ya klabu hiyo kushuka daraja kutoka Ligi Kuu England, huku Steven Gerrard akitajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi yake.(Talksport)
Gerrard, aliyeondoka Al Ettifaq ya Saudi Arabia kwa makubaliano ya pande zote mwaka 2025 baada ya miezi 18, pia anahusishwa na klabu ya Bristol City.(Independent)
Borussia Dortmund inakaribia kufikia makubaliano ya kumrejesha Jadon Sancho majira haya ya kiangazi, ingawa Aston Villa bado ina matumaini ya kumsajili mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 26 atakapokuwa mchezaji huru mwezi Julai. (Teamtalk)
Liverpool inaweza kumkosa winga wa Ivory Coast Yan Diomande, 19, ambaye huenda akabaki RB Leipzig kwa angalau mwaka mmoja zaidi. (Christian Falk via CFBayerninsider)
Chelsea imewaongeza Xabi Alonso na Marco Silva katika orodha ya makocha wanaowania kuinoa klabu hiyo msimu ujao. (Sun)
Bayern Munich itaanza mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa England Harry Kane mwishoni mwa msimu, ikitaka kumbakisha zaidi ya mwaka 2027. (Mirror)
AC Milan na Bayern Munich zote zinamuwania mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic iwapo hataongeza mkataba wake na Juventus majira haya ya kiangazi.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid