Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: City yamtolea macho Enzo Fernandez
Manchester City wanafikiria kumsajili kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernandez (miaka 25), msimu huu wa joto. (Athletic)
Liverpool, Manchester United, Manchester City na Real Madrid wanamfuatilia winga wa AC Milan, Rafael Leao (26), anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mail)
Aston Villa wanamuwania kipa wa Manchester City na England, James Trafford (23), kama mbadala wa Emiliano Martinez (33) iwapo ataondoka. (Times)
Manchester United wanamfuatilia beki wa Tottenham Hotspur, Micky van de Ven (25), pamoja na kiungo wa Brighton & Hove Albion, Carlos Baleba (22). (Athletic)
Manchester City wako mbele katika mbio za kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson (23), licha ya ushindani kutoka kwa Manchester United na Arsenal. (Sky Sports)
Winga wa Manchester United, Jadon Sancho, ambaye yuko kwa mkopo Aston Villa, ameridhia kurejea Borussia Dortmund, huku mazungumzo yakiendelea. (Sky Sport)
Mawakala wa winga wa Ivory Coast, Yan Diomande (19), tayari wamezungumza na Liverpool na Paris Saint-Germain, lakini RB Leipzig wanataka kumbakiza kwa msimu mwingine. (Bild)
Beki wa kati wa Brighton & Hove Albion, Igor Julio (28), anaweza kurejea Brazil huku Cruzeiro wakiangalia uwezekano huo. (ESPN - in Portuguese)
Athletic Club wanatarajiwa kumteua Edin Terzic kuwa kocha mpya kuchukua nafasi ya Ernesto Valverde. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Wolverhampton Wanderers, AFC Bournemouth na Sunderland wanamuwania mshambuliaji wa Queens Park Rangers, Rumarn Burrell (25). (Football Insider)
Brentford wameonyesha nia kwa mshambuliaji wa Dynamo Kyiv, Matviy Ponomarenko (20), kama mbadala wa Igor Thiago (24), anayehusishwa na Chelsea na Tottenham Hotspur. (Teamtalk)
Nottingham Forest wanapanga kumsajili kiungo wa Celtic, Arne Engels (22), baada ya ofa yao ya pauni milioni 25 kukataliwa hapo awali. (Teamtalk)
Tottenham Hotspur wako kwenye mazungumzo na Sebastian Kehl ili awe mkurugenzi mwenza wa michezo baada ya kuondoka Borussia Dortmund. (Sun)