Afisa wa Marekani: Trump hajaridhika na pendekezo la Iran
Afisa mmoja wa Marekani alisema siku ya Jumatatu kuwa Rais Donald Trump hakuridhishwa na pendekezo la Iran la kumaliza vita kwa sababu halikuzungumzia mpango wa nyuklia wa Iran.
Shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa huyo wa Marekani akisema, akimzungumzia Trump: "Hapendi pendekezo hili."
Mapema Jumatatu, Trump alijadili pendekezo hilo na washauri wake wakuu wa usalama wa kitaifa.
Mzozo wa Marekani na Iran umesalia palepale huku usambazaji wa nishati kutoka eneo hilo ukipungua.
Vyanzo vya habari vya Iran vilisema mapema Jumatatu kwamba pendekezo hilo litaahirisha majadiliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran hadi vita vitakapoisha na mizozo inayohusiana na urambazaji kutoka Ghuba kutatuliwa.
Tangu mwanzoni Washington imesisitiza kuwa masuala ya nyuklia lazima yashughulikiwe.
Vyanzo vya habari kutoka Pakistan, vikifanya kazi kama mpatanishi, viliripoti kuwa juhudi za kukomesha uhasama kati ya Marekani na Iran hazijakoma.
Hata hivyo, matumaini ya kufufua mazungumzo ua amani yamefifia tangu Trump atangaze wikendi iliyopita kwamba anaahirisha ziara ya mjumbe wake maalum Steve Wittkopf na mkwe wake Jared Kushner mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan.
Pia unaweza kusoma: