Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ufahamu Mlango Bahari wa Malacca na umuhimu wake kwa biashara ya kimataifa
Wakati Marekani inaendeleza kizuizi chake katika mlango bahari wa Hormuz, kuna njia nyingine muhimu ya bahari imeanza kugonga vichwa vya bahari.
Mlango bahari wa Mallaca, Kusini Mashariki mwa Asia. Maafisa wa Indonesia wameripoti kuwa Marekani imeomba ruhusa kutumia anga zao baada ya kuafikia makubaliano.
Kulingana na Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Indonesia, makubaliano ya mwisho bado hayajaafikiwa.
Wataalam wanasema hatua hiyo itakua na athari katika siasa za jiolojia.
Lakini mlango bahari wa Malacca una umuhimu gani?
Umuhimu wa kimataifa
Azifa Strina mwanafunzi wa uzamifu na mtalaam wa masuala ya kikanda katika chuo kikuu cha Illinois, amefanya utafiti kuhusu matukio ya mlango bahari wa Malacca.
"Mlango bahari wa Mallaca ni muhimu kwasababu ni njia fupi na yenye ufanisi mkubwa ikija katika safari za bahari na huunganisha bahari Hindi na Pacific, na kuifanya muhimu kwa biashara eneo la Mashariki ya Kati, Ulaya, Mashariki mwa Asia" Alisema.
"Njia hii ya bahari huunganisha bahari ya kusini mwa China, ambapo husafirisha theluthi tatu ya biashara zote duniani.
Njia nyembamba ya mlango bahari wa Mallaca ipo eneo la Phillips karibu na Singapore na ina upana wa kilomita 2.8
Kulingana na ripoti kutoka shirika la Marekani la Nishati EIA, mapipa 23.2 ya mafuta hupita eneo hilo kila siku, hii ikuwa 29% ya biashara yote ya mafuta duniani. Eneo hilo pia husafirisha gesi kizio cha ukubwa wa mita millioni 260 kila siku.
Njia hiyo ya bahari pia ni muhimu katika usafirishaji wa bidhaa za kielektroniki, viwanda, bidhaa za kawaida, mashine na magari.
"25% ya biashara yote ya magari duniani hupitia eneo hili, ikiwemo biashara ya chakula kama nafaka,na maharagwe ya soya" Alisema Gokce Balci mhadhiri katika chuo kikuu cha Leeds, Uingereza.
Uharamia pia ni changamoto eneo hili la bahari, kulingana na shirika moja la Singapore ReCap information sharing center, visa 108 vya wizi wa bahari viliripotiwa katika mlango bahari wa Malacca mwaka wa 2025, hii ikiwa idadi ya juu kuwahi kurekodiwa tangu mwaka wa 2007.
Eneo hilo la bahari pia hukubwa na majanga asili kama vile Tsunami iliyoshuhudiwa mwaka wa 2004 na kusababisha uharibu mkubwa wa miundombinu eneo hilo.
Kwa nini eneo hili ni muhimu?
Wataalam wanasema umuhimu wa mlango bahari wa Malacca si tu umuhimu wake wa kusafirisha vitu bali pia nafasi yake katika siasa za dunia.
"Mvutano wowote kati ya China, Marekani na India kuhusu ubabe wa umiliki wa bahari, kunaweza kuathiri eneo hilo la bahari la Malacca." Alisema Gokce Balci.
Azifa Strina anasema uwezekano wa jeshi la Marekani kutumia anga za Indonesia kutakuwa na athari kubwa.
"Naona hili likiathiri mfumo wa kusimamia eneo hilo hata kama haitaathiri biashara mara moja."
"Mfumo huu umeundwa kushughulikia vitisho kama vile uharamia, magendo na uhalifu wa baharini, na si kushindana na mataifa makubwa ya dunia," anasema.
"Hivyo basi, pale taifa kubwa kama Marekani linapoongeza uwepo wake wa moja kwa moja, linazua suala la kiusalama ambao mfumo uliopo kwa sasa haujajiandaa kuushughulikia."
Hata hivyo, kwa muda mfupi, kulingana naye, hakuna misukosuko mikubwa inayotarajiwa.
"Bado sidhani kama usafirishaji wa kibiashara ambao utaathirika, kwa sababu motisha za kuendeleza biashara ni kubwa sana," alisema.
Kulingana naye hatari ipo katika siku za usoni.
"Wasiwasi huu unahusu mwelekeo wa muda mrefu. Ikiwa China itaona hili kama ufuatiliaji wa Marekani au uwekezaji wa kimkakati karibu na njia muhimu ya bahari kama Mlango wa Malacca, inaweza kujibu,si lazima kwa kuzuia biashara, bali kwa kuongeza uwepo au ushawishi wake."
"Hapa ndipo hatari ilipo. Mazingira ya usalama yanaweza kubadilika kutoka mfumo wa ushirikiano na utekelezaji wa sheria hadi ule wa ushindani na kijeshi."
Azifa anaonya kuwa mabadiliko haya yanaweza kuwa na athari halisi hata bila kuwepo kwa mzozo wa moja kwa moja.
Pia anaonya dhidi ya kuitazama nafasi ya Indonesia kwa mtazamo finyu.
"Haipaswi kuonekana kama Indonesia inaegemea upande mmoja," anasema.
"Inaonekana Indonesia inatafuta mkakati wa kusawazisha, ikiimarisha ushirikiano na Marekani, kurejesha uhusiano wao wa kiuchumi na China, na kushirikiana na washirika wengine, wakiwemo Urusi."
Hali tete ya mlango bahari wa Malacca
Mwaka wa 2003, aliyekuwa Rais wa China Hu Jintao alibuni neno "Malacca Dilemma" kuelezea utegemezi mkubwa wa China kwa Mlango bahari wa Malacca.
Kulingana na takwimu kutoka mamlaka ya nishati ya Marekani EIA na mradi wa nishati wa China CSIS, takribani robo tatu ya uagizaji wa mafuta wa China na karibu asilimia 60 ya biashara yake ya baharini hupitia Mlango wa Malacca pamoja na Bahari ya China Kusini.
Hata hivyo, tatizo hili halihusu China pekee.
Kwa mujibu wa Gokce Balci, Japan na Korea Kusini pia zinategemea sana Mlango wa Malacca kwa nishati, ambapo takribani asilimia 90 ya uagizaji wao wa mafuta hupitia njia hiyo.
Anaongeza kuwa njia hii ya maji pia ni muhimu sana kwa Singapore, ambayo ina bandari ya pili kubwa kwa shughuli nyingi zaidi duniani ya makontena, na pia ni kitovu kikuu cha kimataifa cha kujazia mafuta meli.
Kwa mujibu wa Azifa Strina, kupunguza utegemezi wa China kwa Mlango bahari wa Malacca kwa muda mfupi si jambo rahisi kutekeleza.