Tetesi za soka Jumapili: Liverpool yamuwania Beukema wa Napoli

Beukema

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 1

Liverpool wametoa ofa ya kumnunua mlinzi wa kati wa Uholanzi, Sam Beukema (27), kutoka Napoli, ambapo dili hilo linakadiriwa kuwa na thamani ya euro milioni 28 .(AreaNapoli via Teamtalk)

Arsenal, Chelsea na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili winga wa Ureno Rafael Leao (26) kutoka AC Milan, ambaye yuko tayari kukubali ofa ya takriban euro milioni 50.. (The Hard Tackle)

Manchester United wanaweza pia kumfuatilia kiungo wa zamani wa Nottingham Forest, Danilo (25), ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Botafogo nchini Brazil.(Fogao.net via SportWitness, external)

Danilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Roma wako tayari kutumia kipengele cha kumnunua Donyell Malen kutoka Aston Villa kwa euro milioni 25 , baada ya winga huyo wa Uholanzi (27) kufunga mabao 12 tangu ajiunge nao kwa mkopo mwezi Januari. (Voetbal International via Express & Star)

Hata hivyo, Manchester United, Chelsea na Newcastle United pia wanamuwania Malen, ambaye ada yake ya usajili inaweza kufikia euro milioni 30.(Corriere Dello Sport via Manchester Evening News)

Aston Villa na Newcastle United wana nia ya kuwasajili walinda lango James Trafford (23) wa Manchester City na Alex Remiro (31) wa Real Sociedad. (Football Insider, external)

James Trafford

Chanzo cha picha, Getty Images

Goncalo Ramos (24) anataka kuanza mechi nyingi zaidi na anaweza kuondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu, huku vilabu kadhaa vikimuwania mshambuliaji huyo wa Ureno. (Fabrizio Romano)

Leeds United wanataka pauni milioni 10 kwa winga wa Ubelgiji Largie Ramazani (25), ambaye amefunga mabao sita katika mechi zake 13 zilizopita akiwa kwa mkopo Valencia.(Football Insider)