Urusi inaisaidia Iran vipi katika vita vinavyoendelea?

Muda wa kusoma: Dakika 3

Katika uchambuzi wetu wa magazeti tunaangazia taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya kimataifa, tukianza na Wall Street Journal, iliyochapisha taarifa yenye mada "jinsi Urusi inavyoiunga mkono Iran dhidi ya Marekani."

Jarida la Wall street Journal, linaashiria kuwa kuna muungano kati ya Urusi na Iran dhidi ya Marekani.

Gazeti hilo linasema kuwa ingawa Marekani inajua hatari ambayo inaletwa na Iran, anakabiliana katika njia tofauti na Urusi, huku ikitumia ujasusi kujua kiwango cha msaada wa Urusi kwa Iran.

Kulingana na gazeti hilo, mkutano wa hivi karibuni kati ya Rais Vladimir Putin na Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araghchi mjini St Petersburg, zinaendana na uvumbuzi kuwa Urusi imekuwa ikiipa Tehran taarifa za kijasusi ambazo wamekuwa wakitumia kulenga Marekani.

Gazeti moja la Ujerumani lilichapisha kuwa, ujasusi wa Urusi uliipa Tehran taarifa kuhusu vituo vya kijeshi na madini ya urani inayofuatiliwa kwa karibu na setilaiti za Marekani, na hii iliisaidia Iran kuhamisha vituo vilivyokuwa hatarini.

Chapisho hilo pia linaoongezea kuwa Urusi imeiamrisha ndege zisizo na rubani aina ya Shahed, na kuzifanya kuwa zenye nguvu zaidi na vigumu kuzidungua.

Awali naibu rais wa umoja wa ulaya Kaja Kallas, aliwahi kudokeza kuwa ndege zisizo na rubani zinazotumika kushambulia mataifa ya ghuba, zina teknolojia kutoka Urusi.

Inasemakana Urusi imeafikia makubaliano na Iran ya dola million 589, ya kuipa silaha za ulinzi wa angani.

Msemaji wa idara ya ujasusi nchini Marekani aliambia shirika la habari la NBC kuwa kuna uwezekano wa Urusi kuwatuma mafundi wake nchini Iran kusaidia kutengeneza makombora na mifumo ya kurusha makombora hayo.

Kwa kifupi Urusi inaisaidia Iran kwa kuwapa taarifa za kijasusi, kufuatilia picha za setilaiti, kuwapa teknolojia mpya ya ndege zisizo na rubani pamoja na ushauri wa kijeshi.

Ziara ya mfalme Charles nchini Marekani

Katika gazeti la Uingereza la The Guardian, kuna taarifa ambayo ilichapishwa kuhusu ziara ya mfalme Charles nchini Marekani, ambayo mwandishi anaelezea ilikuwa ya kuendeleza uhusiano ambao haujulikani unaenda wapi.

Kulingana na gazeti hilo sakata la Jeffrey Epstein limewaathiri rais wa Marekani pamoja na Ufalme wa Uingereza, suala ambalo limechangia kupunguka kwa imani kwa ufalme huo, huku uungwaji mkono wa Trump pia ukipungua.

Kulingana na taarifa hiyo Ulaya na Uingereza wana ushawishi mdogo sana kwa Marekani na Donald Trump kwa jumla.

Gazeti hilo pia linatabiri vita vya muda mrefu nchini Iran na mashariki ya Kati, huku kukiwa na uwezekano wa kutenguka kwa muungano wa kujihami wa Nato.

Ila ziara ya mfalme Charles ilitoa ishara ya uwepo wa ushikamano wa muda, kati ya Uingereza na Marekani.