Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal yamgeukia Bradley Barcola
Arsenal wamewasiliana na mawakala wa Bradley Barcola 23 huku wakijaribu kuipiku hatua ya Liverpool ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa, kutoka Paris St-Germain. (Give me Sport)
Mshambuliaji raia wa Uingereza Marcus Rashford, 28, amejitolea kufufua kipaji chake Manchester United baada ya kurejea klabuni hapo kufuatia muda wake wa mkopo Barcelona. (Sun)
Aston Villa na Roma wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji raia wa Brazil Endrick, 22, kwa mkopo kutoka Real Madrid. (AS)
Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 33, anatarajiwa kuongeza mkataba wake na Bayern Munich hadi 2029. (Times)
Liverpool inaweza kumwachilia mshambuliaji wa Uholanzi, Cody Gakpo, 27, kujiunga na Tottenham ikiwa watampata mmoja wa wachezaji wanaowalenga. (Football Insider)
Arsenal na Tottenham walionyesha nia ya kumsajili Ferran Torres wa Barcelona kabla ya mshambuliaji huyo wa Uhispania, 26, kuingia katika makubaliano na Paris St-Germain. (TeamTalk)
Crystal Palace wameanzisha mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Senegal, Lamine Camara, 22, kutoka Monaco. (Nicolo Schira)
Manchester United na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia beki wa kushoto wa Club Brugge na raia wa Ubelgiji, Joaquin Seys, 21. (Sun)
Hector Fort 20 ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona msimu huu wa joto, huku Everton na Fulham wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka beki huyo wa kulia wa Uhispania. (TeamTalk)
Fulham wamekubali kumsajili kiungo wa Ireland Kaskazini, Shea Charles, 22, kutoka Southampton katika mkataba wenye thamani ya pauni milioni 30. (Athletic)
Mshambuliaji wa Scotland, Robbie Ure, 22, anatarajiwa kujiunga na Sevilla kutoka kwa vinara wa ligi ya Sweden, IK Sirius kwa euro milioni 9 (£7.7m). (ESPN)
Sheffield United imetoa ofa bora ya pauni milioni 8 kwa beki wa kati wa Leicester City na Australia, Harry Souttar, 27. (Football Insider)