Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tume ya uchunguzi yasema watu 518 walifariki dunia wakati wa ghasia za uchaguzi Tanzania
Tume imesema idadi hyo inaweza kuwa kubwa zaidi kwani Tume inasema kuwa kuna uwezekano kuwa baadhi ya familia zimezika wapendwa wao bila kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ya afya au hawakupata fursa ya kuja mbele ya tume.
Muhtasari
- Wachambuzi wagawanyika kuhusu chanzo cha vurugu na uwajibikaji nchini Tanzania
- Raia wa Tanzania aliyekimbilia Zambia ahoji ufanisi wa ripoti ya matukio ya Oktoba 29
- CHADEMA yapinga ripoti ya tume ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29
- 'Chombo kitakachoundwa kitaangazia taarifa za wanaodaiwa kutekwa ambao bado hawajapatikana'
- 'Hii ni ripoti ya rais' - rais Samia
- 'Bado tunajifunza na kukua katika mfumo wa demokrasia'- Samia Rais
- Tume ya Uchunguzi yatoa mapendekezo kwa serikali
- Haiwezekani mtu ambaye si Mtanzania awe na uchungu kuliko watanzania - rais Samia
- Madai ya uwepo wa makaburi ya halaiki hayana ushahidi – Tume
- Idadi ya majeruhi wa wakati wa vurugu yatajwa
- Kuna madai ya watu kuuawa katika nyumba zao – Tume
- Idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi
- 'Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni'
- Tume ya uchunguzi yasema watu 518 walifariki dunia wakati wa ghasia za uchaguzi Tanzania
- Tume yasema matukio ya vurugu yalifadhiliwa
- Vyanzo vya ghasia: Tume yabainisha vyanzo vitano na vichocheo
- Mashambulizi ya Marekani na Israel kitovu cha ukosefu wa usalama Ghuba, Hormuz - Iran
- Lebanon yaishutumu Israel kwa kumshambulia mwandishi wa habari na kumuua
- Afisa mwingine wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani aachia ngazi
- Mamlaka zisitumie haki kama chombo cha kutolea adhabu pekee - Papa Leo
- Hormuz haitafunguliwa kutokana na ukiukaji wa usitishaji vita - Iran
- Serikali ya Zambia yachukua mwili wa rais wa zamani baada ya mvutano na familia
- Mbivu na Mbichi za matukio ya Oktoba 29 kujulikana leo Tanzania
Moja kwa moja
Na Martha Saranga, Rashid Abdallah, Ambia Hirsi & Mariam Mjahid
Mahakama ya Afrika Kusini yaamuru Zambia kurejesha mwili wa rais wa zamani
Mahakama ya Afrika Kusini imetoa amri ya kuurudisha mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu, nchini humo, muda mfupi baada ya serikali ya Zambia kutangaza kuwa imechukua rasmi mwili wake.
Hatua hiyo imekuja saa chache tu baada ya serikali ya Zambia kusema kuwa imepokea mwili wa Lungu, ambaye alifariki akiwa Afrika Kusini, katika kile kinachoonekana kuwa mabadiliko mapya katika mvutano wa muda mrefu kuhusu mazishi yake.
Kesi hiyo imechochewa na mzozo wa kisiasa na kifamilia uliodumu kwa takribani miezi kumi kati ya Lungu na mrithi wake, Rais Hakainde Hichilema.
Serikali ya Zambia imekuwa ikisisitiza kuwa, kama kiongozi wa zamani wa nchi, Lungu anapaswa kupewa heshima ya kitaifa na kuzikwa katika eneo maalum la mazishi ya marais katika mji mkuu Lusaka, pamoja na waliomtangulia.
Hata hivyo, familia ya Lungu ilitaka mazishi ya faragha baada ya mazungumzo na serikali kuhusu maandalizi ya mazishi kuvunjika.
Mwaka uliopita, Mahakama Kuu ya Pretoria ilitoa uamuzi ulioruhusu serikali ya Zambia kuurejesha mwili huo na kuandaa mazishi ya kitaifa, uamuzi uliowashtua na kuwahuzunisha sana wanafamilia wa Lungu mahakamani.
Familia ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, lakini katika taarifa ya kushangaza usiku wa Jumatano, serikali ya Zambia ilisema mwili wa Lungu “umekabidhiwa rasmi” kwa serikali kufuatia hatua za mahakama ya Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uhamisho huo ulifanyika baada ya familia kushindwa kuendeleza kesi yao katika mahakama ya rufaa.
Hata hivyo, saa chache baadaye, mahakama hiyo hiyo ya Afrika Kusini iliamuru serikali ya Zambia kurejesha mwili huo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa tena tarehe 21 Mei.
Soma zaidi:
Raia wa Tanzania aliyekimbilia Zambia ahoji ufanisi wa ripoti ya matukio ya Oktoba 29
Raia mmoja wa Tanzania aliyekimbilia Zambia ameiambia BBC kuwa ripoti hiyo huenda isilete mabadiliko yoyote, akiongeza kwamba atafikiria kurejea nyumbani iwapo tu kutakuwa na uhakika wa wazi wa usalama kwa walioko uhamishoni.
Amina Hassan, si jina lake halisi kwa hofu ya usalama wake ameiambia BBC kuwa ''kupata ripoti ni jambo moja lakini utekelezaji wa mapendekezo yake ni changamoto nyingine''.
Aidha ametilia shaka utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29.
''Ripoti nyingi huleta matumaini, lakini utekelezaji wake huwa tatizo'', akiongeza kuwa ahadi ya katiba mpya imewahi kutolewa hapo awali bila kutekelezwa.
Soma zaidi:
'Chombo kitakachoundwa kitaangazia taarifa za wanaodaiwa kutekwa ambao bado hawajapatikana'
Rais Samia amesema chombo maalum cha upelelezi kitakachoundwa kwa ajili ya kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na tume kitajielekeza kuangazia masuala kadhaa ikiwemo masuala ya wanaodaiwa kutekwa ambao taarifa zao bado hazijapatikana.
Aidha chombo hicho kitaangalia na kubaini waliohusika kuratibu kupanga na kufadhili matukio ya ghasia za Oktoba29.
'Vilevile watajielekeza kubaini matukio ya vurugu na uhalifu,kwa bahati nzuri picha zipo'alieleza
Pia chombo hicho kitaangazia miili ambayo haijapatikana na walioathirika nje ya maeneo ya vurugu.
Soma zaidi:
'Hii ni ripoti ya rais' - rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu amesema ripoti ya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 ni ya rais aliyeunda tume husika.
Akizungumza baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa ripoti hiyo alisema 'Tumesikia masuala yaliyobainishwa na tume'
Hii ni ripoti ya rais kwahiyo wasitokee watu wengine wakadai ownership ya ripoti hii'
Aidha ameahidi kuanza kufanyia kazi mara moja mapendekezo yaliyotolewa na tume hiyo.'Katika muda mfupi ujao serikali itaunda tume ya maridhiano ikijumuisha wadau wote muhimu ili kuziba mianya na kurejesha umoja wa kitaifa.
Soma zaidi:
'Bado tunajifunza na kukua katika mfumo wa demokrasia'- Samia Rais
Rais Samia amesema bado Tanzania inajifunza na kukua katika mfumo wa vyama vingi.
'Demokrasia haina budi kujengwa kwa kuzingatia mazingira ya nchi mila tamaduni za nchi husika nakuongeza kuwa kwa misingi hiyo ‘tuachwe tujenge demokrasia yetu kwa desturi yetu mila na tamaduni zetu'
Ndugu zangu mliponikabidhi dhamana ya kuongoza nchi nilibaini kuwepo kwa changamoto katika mifumo ya demokrasia ya vyama vingi nchini.
Rais Samia amerejelea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa siasa kuhusu kunyimwa uhuru wa kisiasa, uhuru wa kujieleza na changamoto katika mifumo ya uchaguzi akieleza kwamba kupitia falsafa ya 4R hatua kadhaa zilichukuliwa ikiwemo kuundwa kwa kikosi kazi cha kushughulikia changamoto hizo.
Unaweza kusoma Pia:
Tume ya Uchunguzi yatoa mapendekezo kwa serikali
- Kutenga siku ya maombelezi ya kitafa, kuwakumbuka Watanzania waliofariki kwenye ghasia za wakati na baada ya uchaguzi mkuu
- Serikali iweke utaratibu kwa waliopata majeraha kupata usaidizi, ikiwemo viungo bandia
- Serikali iweke mkakati wa kutoa huduma za kisaikolojia katika maeneo yaliyoathirika
- Katiba mpya ipatikane ili itumike katika chaguzi zijazo
- Kuunda tume ya maridhiano ya kitaifa katika nyanya za kijamii, kisiasa na kiuchumi
- Kuundwe baraza la wazee ili kuisaidia tume ya maridhiano
- Sheria ya tume huru ya uchaguzi itekelezwe kwa ukamilifu, ili kuondoa malamakio ya vya vya siasa kuhusu uhuru wa tume
- Kuunda tume ya kijinai ili kuchunguza matukio ya jinai ya wakati wa vurugu za uchaguzi mkuu
- Jeshi la polisi liunde utaratibu wa kurudisha mahusiano na wananchi
- Serikali na vyombo dola vitekeleze majuku yake kwa kuzingatia uwazi na mfumo wa Kidemokrasia wa vyama vingi vya siasa
- Maadili ya viongozi yasimamiwe, ili kudhibiti ufisadi na rushwa Baraza la vijana liundwe ili kuleta maridhiano na kushughulikia mambo ya vijana
Maelezo zaidi:
Madai ya uwepo wa makaburi ya halaiki hayana ushahidi – Tume
Kuna taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vya nje na mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa makaburi ya halaiki katika eneo la Kondo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Tume ilitembelea eneo hilo na kupata taarifa kutoka kwa maafisa na kushirikisha watalaamu mbalimbali ili kufanya uchunguzi wa kisayansi.
Uchunguzi wa tume umegundua kuwa madai ya uwepo wa makaburi ya halaiki hayawezi kuthibitishwa.
Maelezo zaidi:
Kuna madai ya watu kuuawa katika nyumba zao – Tume
Tume imepokea madai kutoka kwa waathirika na mashahidi kuwa kuna watu waliuawa au kujeruhiwa katika maeneo ambayo hayakuwa na ghasia wala vurugu.
Kuna madai ya watu kupigwa risasi katika nyumba makazi yao, ikiwa pamoja na ndani ya nyumba, sebuleni au ndani ya maduka.
Hizi ni tuhuma nzito za uwezekano wa matumizi ya silaha nzito kinyume na sheria za kimataifa na kikanda.
Idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi
Tume imebaini kuwa kuna uwezekano kuwa badhi ya familia zimezika wapendwa wao bila kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ya afya au hawakupata fursa ya kuja mbele ya tume.
Tume pia inasema inawezekana kuwepo kwa majeruhu ambao walitbiwa nje ya mfumo rasmia na taarifa zao kutofikishwa katika vituo rasmia.
Tume pia imepokea taarifa za watu kupotea au kutopatikna tangu wakati wa matukio ya vurugu za uchaguzi mkuu.
Tume pia imepokea ushahidi kuwa watu 39 ambao familia ziliona miili ya wapendwa wao katika hospitali na vituo vya afya, na kutambuliwa lakini miili hiyo baadaye haikuonekana tena.
Kwa kuzingantia hayo idadi ya vifo vya watu 518 inaweza kuwa sio idadi kamili ya waliofariki.
Pia unaweza kusoma:
'Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni'
Baadhi ya waathiriwa wa vurugu hizo waliopoteza wapendwa wao wameeleza hisia zao kwa BBC, wakisimulia maumivu, hofu na matumaini waliyonayo kufuatia tukio hilo.
Mwanaume huyu tumehifadhi utambulisho wake alimpoteza kijana wake aliyefariki dunia kutokana na majeraha ya risasi aliyopata alipokuwa akitoka katika shughuli zake.'kijana wangu ameniachia mtoto mdogo' anayenitegemea.
Kwa upande mwingine wake Mwanaume huyu anasema ripoti hii inamkumbusha machungu ya kumpoteza mke wake wa ndoa.'Nina wakati mgumu,tangu oktoba 30 nilimpoteza mke wangu wa ndoa'
'Alipigwa risasi akiwa dukani kwake amekaa,nilimkuta ameshafariki dunia' alieleza. Wasamaria walinisaidia kumpeleka hospitali.Ripoti hii haina maana yoyote kwangu ikiwa hatutapata haki'.
Maelezo zaidi:
Tume yataja malengo ya walioshiriki katika vurugu
Kuzuia uchaguzi: Lengo kuu ni kvurugu na kuzuia uchaguzi, lengo hili linathibitshwa na matukio mbali mbali, ikiwemo kushambulia askari, mawakala na wasimamizi wa uchaguzi, kuharibu mali za wasimamizi, vitisho, kuvamia vituo vya uchaguzi, kupora mali, kutishia waliojitokeza kupiga kura na waliopiga kura kukakwa au kujaribiwa kukatwa vidole.
Kufikisha ujumbe: Tume inasema miongoni mwa walioshiriki katika vurugu ilikuwa ni kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa serikali, tume inasema vijana walioshiriki walipata mwanya wa kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa wanataka kusikilizwa.
Wizi na uporaji: Miongoni mwa wafanya ghasia, walijitokeza makundi ya waliopora mali na kuiba. Uporaji ulitokea katika maduka na maeneo mengine ya biashara yaliyotembelewa na tume.
Soma zaidi:
Mbinu 16 zilitumika kufanikisha ghasia na vurugu - Tume
Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025, chini ya Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mohamed Chande, amesema takaribani mbinu kumi na sita zilitumika wakati wa kutekeleza vurugu hizo.
Akitaja baadhi ya mbinu hizo amesema, kuweka vizuiz barabarani, kuchoma moto, matumizi na ishara mbali mbali za kutambuliana, matumizi ya pikipiki, kufanya ghasia katika maeneno mengi kwa wakati mmoja.
Tume yasema matukio ya vurugu yalifadhiliwa
Tume imepata ushahidi kuwa matuko ya vurugu yalipangwa, yaliratibiwa, yalifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo.
Waratibu walitumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kuwasajili vijana.
Tume hiyo inasema waratibu hao walikuwa wakizunguka maneno mbalimbali katika vyuo vikuu, masoko na vituo vya mabasi, na kuwaandikisha watu ili kushiriki katika ghasia za Oktoba 29.
Tume inasema waratibu hawakumamatwa kwa sababu hawakuwepo wakati wa vurugu.