Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Gyökeres sehemu ya ofa ya kumsajili Álvarez
Viktor Gyökeres anaweza kutumika kama sehemu ya makubaliano ya kumleta Julián Álvarez Arsenal, Liverpool imewasiliana na Paris Saint-Germain kuhusu Bradley Barcola, huku nahodha wa Tottenham, Cristian Romero, akitarajiwa kuondoka klabuni.
Arsenal inafuatilia uwezekano wa kumtoa mshambuliaji wa Uswidi, Viktor Gyökeres, 28, kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Argentina wa Atletico Madrid, Julián Álvarez, 26. (Talksport)
Barcelona itarejea katika mbio za kumsajili Álvarez baada ya Kombe la Dunia na huenda pia ikamjumuisha mmoja wa wachezaji wake katika makubaliano hayo. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Barcelona wanataka kumpa mshambuliaji wa Hispania Ferran Torres, 26, mkataba mpya huku Paris Saint-Germain ikivutiwa naye lakini wanapanga kusubiri hadi Septemba kwa sababu ya kanuni za kifedha. (Mundo Deportivo)
Liverpool imeanzisha mawasiliano mapya na Paris Saint-Germain kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Bradley Barcola, 23, katika dirisha hili la usajili. (TeamTalk)
Arsenal inajaribu kumuuza mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, huku AC Milan ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyoongoza katika mbio za kutaka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 29. (TeamTalk)
Sunderland ipo mbioni kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa Ubelgiji Thomas Meunier kufuatia kuondoka kwake Lille. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo hivi karibuni. (Athletic - subscription required)
Liverpool imekataa ofa mpya ya Inter Milan kwa ajili ya Curtis Jones, huku dau lililoboreshwa la takriban pauni milioni 27 likishindwa kufikia kiasi cha pauni milioni 30 ambacho Liverpool inakitaka kwa kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 25. (Talksport)
Everton imeongeza juhudi zake za muda mrefu za kumsajili beki wa kulia wa Genoa na timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Brooke Norton-Cuffy, baada ya kufanya mazungumzo mapya kuhusu uwezekano wa uhamisho wake. (TeamTalk)
Nahodha wa Tottenham Hotspur, Cristian Romero, 28, anatarajiwa kuondoka klabuni msimu huu wa joto, huku Barcelona ikionyesha nia ya kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Argentina. (Talksport)
Mawakala wa Crysencio Summerville wamekutana na Roma kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24 kujiunga nao akitokea West Ham. (Corriere dello Sport - in Italian)
Kipa wa Marekani Gabriel Slonina, 22, kwa sasa yuko kwenye majaribio na Strasbourg, huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia huko akitokea Chelsea. (L'Equipe - in French)