Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Arsenal inamuwania Álvarez wa Argentina

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julián Álvarez, Aston Villa imeiteka Newcastle United katika mbio za kumsajili Johan Manzambi, huku Pep Guardiola akitajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaowania kuteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia.

Arsenal inaendelea kufanya juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Atlético Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julián Álvarez, mwenye umri wa miaka 26, kabla ya maandalizi ya msimu mpya kuanza. (Independent)

Aston Villa inakamilisha hatua za usajili wa kiungo wa Freiburg na timu ya taifa ya Uswisi, Johan Manzambi, 20, ambaye awali alikuwa akielekea kujiunga na Newcastle United. (Athletic - requires subscription)

Wakati huohuo, aliyekuwa kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, 57, ametajwa kuwa miongoni mwa majina yaliyowekwa kwenye orodha ya kuwania nafasi ya kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia, baada ya Paolo Maldini kuteuliwa kuwa mkuu wa masuala ya ufundi wa soka nchini humo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Bayern Munich inaendelea kuwa na imani kuwa itamshawishi mshambuliaji wa England, Harry Kane, 32, kusaini mkataba mpya wa muda mrefu licha ya kuongezeka kwa mvuto kutoka kwa baadhi ya vigogo wa Ulaya, akiwemo Real Madrid. (TeamTalk)

Mlinzi wa Sassuolo, Tarik Muharemović, bado anawindwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England, huku Newcastle United, Sunderland, Leeds United na Bournemouth zote zikionyesha nia ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia na Herzegovina mwenye umri wa miaka 23. (Corriere dello Sport via Football Italia)

Chelsea inafuatilia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, 22, baada ya Liverpool na Manchester United kupunguza hamasa yao ya kumwania nyota huyo. (Caught Offside)

AS Roma inamuwania winga wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, 22. Aidha, klabu hiyo ya Serie A pia inaonyesha nia ya kumsajili winga wa kimataifa wa Ubelgiji, Diego Moreira, 21, anayecheza katika klabu dada ya Chelsea, Strasbourg. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kipa wa Manchester United raia wa Jamhuri ya Czech, Radek Vitek, 22, anawindwa na Celtic baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia alipokuwa kwa mkopo katika klabu ya Bristol City msimu uliopita. (Football Insider)

Atalanta imeanza mazungumzo na kiungo wake Mbrazil, Ederson, 27, kuhusu kuongeza mkataba wake baada ya mpango wa kuhamia Manchester United kuvunjika. Hata hivyo, Newcastle United bado inaendelea kumfuatilia kiungo huyo. (L'Eco di Bergamo - in Italian)

Sunderland inalenga kumfanya winga wa AS Roma raia wa Argentina, Matías Soulé, 23, kuwa usajili wake wa kwanza katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Nyota huyo anakadiriwa kuwa na thamani ya takribani euro milioni 35 (pauni milioni 30). (Northern Echo)

Wakati huohuo, Newcastle United imeanza mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumsajili kipa wa Parma na timu ya taifa ya Japan, Zion Suzuki, 23, huku ikitafuta kipa mpya wa chaguo la kwanza.

Aidha, Tottenham Hotspur na Newcastle United zote zinaonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Misri, Omar Marmoush, 27. (TeamTalk)