Tetesi za soka Ulaya: Arsenal, Barcelona zinamfukuzia Bernardo Silva

Bernardo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bernardo Slva
Muda wa kusoma: Dakika 2

Vilabu vya Arsenal na Barcelona vinaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Ureno, Bernardo Silva, mwenye miaka 31, pindi atakapoondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (ESPN Brazil)

Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Randal Kolo Muani mwenye umri wa miaka 27, kama mbadala wa Mohamed Salah, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Juventus kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain. (Gazzetta dello Sport)

Manchester United wanawafuatilia kiungo wa England anayechezea Nottingham Forest, Elliot Anderson, mwenye miaka 23, pamoja na kiungo Mfaransa wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni, mwenye miaka 26, kama mbadala wa Casemiro anayeondoka. (Telegraph)

Brighton & Hove Albion wanaweza kumpa mlinda mlango wa England, James Trafford, mwenye miaka 23, nafasi ya kuondoka Manchester City majira ya joto kwa kumsajili (Florian Plettenberg)

Kobbie Mainoo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kobbie Mainoo

Kiungo wa England, Kobbie Mainoo, mwenye miaka 21, amekubali kufanya mazungumzo ya mkataba mpya wa miaka mitano na Manchester United. (The Sun)

Manchester United na Galatasaray wako tayari kuwania saini ya kiungo wa Uholanzi wa Juventus, Teun Koopmeiners, mwenye miaka 28. (Tuttosport)

Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji chipukizi wa Palmeiras, Eduardo Conceicao, mwenye miaka 16, huku Manchester City, Manchester United na Newcastle United pia zikionesha nia. Hata hivyo, hatoweza kuhamia Ulaya hadi atakapofikisha miaka 18 mwaka ujao. (TeamTalk)

West Ham United wako tayari kumuuza beki wa Ugiriki, Konstantinos Mavropanos, mwenye miaka 28, majira ya joto huku vilabu vya Bundesliga vikimwania, lakini wanahitaji ada kubwa. (Football Insider)

Chelsea na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, mwenye miaka 22. (Caught Offside)

Leeds United wanapanga kumpa mkataba mpya kiungo wa Wales, Ethan Ampadu, mwenye miaka 25, mwishoni mwa msimu. (TeamTalk)