Tetesi za soka Ulaya: Bayern Munich kumzuia Olise kupitia donge nono

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Bayern Munich wanapanga kuongeza mara mbili ya mshahara wa kiungo wa kati wa Ufaransa Michael Olise kama sehemu ya makubaliano ya kumuweka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika klabu hiyo hadi 2031. (Christian Falk)

Manchester United na Arsenal wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bournemouth na England Alex Scott, 22, lakini uhamisho wowote wenye mafanikio unaweza kugharimu takriban £60m. (Mail)

Arsenal pia wanawasiliana na Leicester City kuhusu dili la winga wa chini ya miaka 19 wa England Jeremy Monga, huku The Gunners wakipanga kulipa ada ya haki kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16 na kuepuka mahakama. (Athletic - Team- Talks)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alex Scott

Real Madrid wataanzisha mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa mchezaji wao wa kimataifa wa Argentina Enzo Fernandez, 25, baada ya kumfanya kuwa mlengwa wao mkuu wa kiungo msimu huu. (AS)

Aston Villa wameonyesha nia ya kutaka kumnunua winga wa West Ham na England Jarrod Bowen, 29, lakini makubaliano yanaweza kuwa magumu hadi Villa ifanye mauzo ya wachezaji. (Athletic - Subcsription Required)

Aston Villa pia wameweka wazi kwa vilabu vinavyovutiwa kuwa hawataki kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers mwenye umri wa miaka 23 msimu huu. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha, Brighton.com

Maelezo ya picha, Said el Mala

Newcastle United inaonesha nia ya kutaka kumnunua winga wa Cologne na Ujerumani chini ya umri wa miaka 21 Said El Mala, 19, na katika kuwasiliana na fowadi wa Lille na Ubelgiji Matias Fernandez-Pardo, 21.

Lakini Liverpool pia wanasubiri kutoka pembeni ikiwa watashindwa kumpata winga wa RB Leipzig na Ivory Coast Yan Diomande, 19, au mshambuliaji wa Paris St-Germain, na Ufaransa Bradley.

Arsenal wanaendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 26. (TeamTalks),

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erling Halaand

Real Madrid wanavutiwa na mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 25, iwapo winga wa Brazil Vinicius Jr, 25, ataondoka Bernabeu. (Sport - Spanish)

Manchester United wanatarajiwa kuzindua mbinu rasmi ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Ureno Mateus Fernandes, 21, siku zijazo. (TeamTalks).

Beki wa Borussia Monchengladbach na Uswizi Nico Elvedi, 29, yuko tayari kuhamia Leeds United. (Football Insider)

Aston Villa wako kwenye mazungumzo na Flamengo kuhusu kumsajili beki wao wa miaka 27 raia wa Brazil Emerson Royal. (Sports)