Tetesi za soka Jumatano: Chelsea, Arsenal, Tottenham zamuwania Rashford

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Tottenham Hotspur, Chelsea na Arsenal zinadaiwa kupanga kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford (28). Hata hivyo, viongozi wa Manchester United hawataki kumuuza kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu ya England.

Mlinda lango wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martínez (33), anawindwa na Juventus, huku Arsenal ikimfuatilia beki wa Aston Villa na England, Ezri Konsa (28).

Nottingham Forest ipo katika mazungumzo ya hatua za mwisho kumsajili beki wa Sporting CP na Ivory Coast, Ousmane Diomande (22).

Beki wa kati wa West Ham United, Jean-Clair Todibo (26), anahusishwa na uhamisho kwenda Juventus.

Manchester United bado inatafuta kiungo wa kati, lakini imepunguza nia ya kuwasajili Carlos Baleba (22) wa Brighton na Alex Scott (22) wa Bournemouth kutokana na gharama kubwa za usajili wao.

Bournemouth imeazimia kumbakisha Alex Scott licha ya mchezaji huyo wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 kukataa kusaini mkataba mpya. Arsenal inaendelea kumfuatilia.

Ipswich Town imefikia makubaliano ya awali kumsajili mshambuliaji wa Celtic na Japan, Daizen Maeda (28), kwa ada ya pauni milioni 8 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 2 kulingana na mafanikio.

Beki wa kulia wa Manchester United, James Overy (18), raia wa Australia, anafuatiliwa na Rangers pamoja na klabu kadhaa kutoka Australia.