EU yatangaza mpango wa kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa walio chini ya miaka 15
Umoja wa Ulaya umetangaza mipango ya kuzuia watoto walio chini ya umri wa miaka 15 kutumia mitandao ya kijamii katika nchi wanachama, katika juhudi za kuboresha ustawi wao na kukabiliana na changamoto za usalama mtandaoni.
Chini ya mipango hiyo, kutakuwa na hatua za taratibu kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na watoto, ikiwemo kuwapiga marufuku walio chini ya miaka 13 kufikia majukwaa hayo.
Watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 15 wataruhusiwa kutumia majukwaa hayo kwa muda wa saa moja pekee kwa siku kupitia "akaunti ndogo" zitakazofunguliwa kupitia akaunti ya mzazi au mlezi wao.
Tume ya Ulaya imesema kampuni za mitandao ya kijamii zitapaswa kuthibitisha kwamba majukwaa yao yameundwa kwa kuzingatia usalama, au zitakabiliwa na faini ya hadi asilimia 6 ya mapato yao ya kimataifa. Mkuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, alisema hatua hiyo "itawarudishia wazazi udhibiti".
Aliongeza kuwa sheria hiyo, inayojulikana kama EU Kids Act, itawapa wazazi "zana za kuwasaidia watoto wao kuzunguka katika ulimwengu salama zaidi".
Vikwazo hivyo havitaathiri tu programu zinazojulikana kama TikTok, Instagram na Snapchat, bali pia YouTube na majukwaa mengine ya kushirikiana video, pamoja na chatbots za AI na michezo ya mtandaoni.
"Watoto wengi wanaoneshwa mapema mno ulimwengu wa mtandaoni ambao hawajawa tayari kukabiliana nao, mazingira ambayo uonevu unaweza kukufuata hadi nyumbani, na ambapo kila kosa linaweza kurekodiwa milele," alisema von der Leyen.
Chini ya sheria hiyo, ni watoto wenye umri wa miaka 15 na zaidi pekee watakaoruhusiwa kufungua akaunti zao wenyewe kwenye mitandao ya kijamii.
Unaweza kusoma;