Moja kwa moja, Risasi zasikika Washington, Trump aokolewa na walinzi

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, mtu mwenye silaha alivamia hafla ya chakula cha jioni iliyohudhuriwa na Trump na mkewe, na kufyatua risasi kuelekea maafisa wa usalama katika eneo la ukaguzi kabla ya kuingia ukumbini.

Moja kwa moja

Na Yusuph Mazimu

  1. Picha mbali mbali za tukio la risasi Washington

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mmoja wa maafisa wakubwa wa Ikulu ya White House Stephen Miller akimsaidia mkewe Katie Miller kwenye tukio hilo la risasi Washington. Rais Donald Trump, pamoja na maafisa wengine wa serikali, waliondolewa kutoka hoteli ya Washington Hilton baada ya risasi kuanza kusikikia
    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watu wa usalama walidhibiti eneo la tukio mara moja
    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    a

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance akiondolewa na yeye kuelekea kwenye eneo salama
    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

  2. Mshukiwa wa tukio la risasi Washington atambuliwa na atafikishwa Mahakamani kesho

    s

    Chanzo cha picha, Donald Trump/ Truth Social

    Maelezo ya picha, Trump alichapisha picha hii kwneye mtandao wake wa Truth Social kumuonyesha mchukiwa

    Mamlaka za Marekani zimetambua mshukiwa wa tukio hilo kuwa ni Cole Tomas Allen, mwenye umri wa miaka 31 kutoka Torrance, California. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu kujibu mashtaka yake.

    Mwanasheria wa kutoka eneo la Columbia, Marekani, Jeanine Pirro, amesema anakabiliwa na makosa ya kutumia silaha katika uhalifu wa vurugu pamoja na kushambulia maafisa wa serikali kwa kutumia silaha hatari.

    Amesema kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya shirikisho, na hatua za kisheria tayari zimeanza kuchukuliwa dhidi yake.

    Polisi wamesema bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo, lakini mshukiwa alikamatwa eneo la ukaguzi lililowekwa kwa usalama wa hafla hiyo.

  3. Mshukiwa wa tukio la risasi Washington alikuwa mgeni wa hoteli, polisi wasema

    s

    Chanzo cha picha, Reuters

    Polisi wa Washington DC wamesema mshukiwa wa tukio la kufyatua risasi katika hafla ya Waandishi wa Habari wa Ikulu Marekani, alikuwa mgeni katika hoteli iliyokuwa mwenyeji wa hafla hiyo.

    Kiongozi mwandamizi wa Polisi, Jeff Carroll, amesema chumba chake kimeshikiliwa kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea.

    Amesema mshukiwa huyo hakuwahi kujulikana na polisi kabla ya tukio hilo, na hakuna ishara ya awali iliyokuwa ikionyesha hatari yoyote.

    Polisi pia wamesema eneo la ukaguzi lililopo kwenye mlango wa tukio hilo lilisaidia kumkamata mshukiwa haraka mara baada ya tukio.

    Aidha, mamlaka zimesema kwa sasa hakuna dalili za kuwepo kwa tishio lingine kwa umma.

  4. Risasi zasikika Washington, Trump aokolewa na walinzi

    s

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump waliondolewa haraka kwenye hafla ya kila mwaka ya chakula cha jioni ya waandishi wa habari (White House Correspondents’ Dinner) mjini Washington DC baada ya mtu mwenye silaha kuvamia na kufyatua risasi karibu na eneo la usalama.

    Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, mshukiwa huyo alifyatua risasi kuelekea maafisa wa usalama katika eneo la ukaguzi kabla ya kuingia ukumbini. Afisa mmoja alipigwa risasi lakini hakupata madhara makubwa kutokana na kuvaa kuizuia risasi na hali yake inaelezwa kuwa nzuri.

    s
    Maelezo ya picha, Wageni wengi walijificha chini ya meza kukwepa risasi

    Washiriki wa hafla hiyo, wakiwemo viongozi wa serikali na wanahabari, walilazimika kujificha chini ya meza huku vikosi vya usalama vikichukua hatua za haraka kumdhibiti mshukiwa huyo.

    Mshukiwa huyo, aliyekuwa na silaha kadhaa, alikamatwa na mamlaka na anaaminika kuwa alitenda tukio hilo akiwa peke yake. Hakuna viongozi wa serikali walioumia katika tukio hilo.

    Baada ya tukio hilo, Trump aliwashukuru maafisa wa usalama kwa hatua zao za haraka na kusema tukio hilo linachunguzwa zaidi huku sababu za mshambulizi bado hazijajulikana.

    Hafla hiyo, iliyokuwa imehudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi wakuu wa serikali, ilisitishwa kufuatia tukio hilo la ghafla la kiusalama.

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Halfa ilianza kwa utulivu Trump na mkewe wakihudhuria kabla ya kuhairishwa baadaye
  5. Karibu katika habari zetu za moja kwa moja leo Jumapili Aprili 26, 2025