Mgomo wa wahudumu wa usafiri wa umma wasitishwa Kenya

Kwa sasa bei ya mafuta imeshuka kwa shilingi 10 huku bei ya mafuta taa ikipanda kwa shilingi 38 ilhali bei ya petroli ikisalia jinsi ilivyo.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula, Asha Juma & Ambia Hirsi

  1. Tunakomea hapo kwa leo. Kwaheri.

  2. Miili ya Waitaliano wawili waliokufa maji yapatikana kwenye pango Maldives

    ,

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Miili ya Waitaliano wawili waliokufa maji katika ajali ya kuzamia majini katika eneo la Maldives wiki jana imetolewa hadharani, maafisa wa eneo hilo wameiambia BBC.

    "Waliopolewa kutoka chumba cha tatu cha pango la chini ya maji na wapiga mbizi mtaalamu kutoka Finland baada ya operesheni ya saa mbili," Msemaji wa serikali ya Maldeves, Mohamed Hossain Shareef,aliiambia BBC.

    Miili hiyo miwili ilikuwa imepelekwa mji mkuu wa wa nchi hiyo kwa ajili ya kutambuliwa.

    Walikuwa miongoni mwa watu watano waliofariki katika ajali hiyo.

    Mwili wa kwanza wa mzamiaji wa Kiitaliano, ambaye alikuwa mwanachama wa kikundi hicho, ulipatikana muda mfupi baada ya ajali kutokea siku ya Alhamisi.

    Ametajwa na vyombo vya habari vya Italia kama meneja wa uendeshaji wa boti na mkufunzii wa kupiga mbizi Gianluca Benedetti.

    Wapiga mbizi hao wanne waliotoweka hatimaye walipatikana na wapiga mbizi wenzao siku ya Jumatatu kwenye pango lililokuwa mbali zaidi na lango la kuingilia.

    Inajulikana ndani kama "pango la papa", lina kina cha urefu wa hadi mita 60 sawa na (futi 197).

    Shughuli ya kutafuta miili miwili iliyosalia itaanza tena Jumatano na mamlaka za Maldives zina matumaini kwamba itapatikana siku hiyo hiyo.

  3. Enzo Maresca kumrithi Guardiola Man City

    Enzo Maresca

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Enzo Maresca aliondoka Chelsea mnamo Januari chini ya miezi sita baada ya kushinda Kombe la Dunia la Vilabu

    Enzo Maresca anatarajiwa kuchukua nafasi ya Pep Guardiola kama meneja wa Manchester City kabla ya msimu ujao.

    Kama tulivyoripoti Jumatatu mkufunzi mashuhuri wa City Guardiola anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kufuatia mchezo wa Jumapili dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Etihad, mechi yao ya mwisho msimu huu.

    Kocha mkuu wa zamani wa Chelsea Maresca anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mhispania huyo maarufu kwa msimu wa 2026-27.

    Huku City wakijiandaa na kuondoka kwa Guardiola majira ya kiangazi kwa zaidi ya miezi sita, mazungumzo na Maresca yako katika hatua nzuri.

    Kocha huyo aliye na umri wa miaka 46 anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mrithi wa Guardiola muda utakapowadia.

    Mtaliano huyo ambaye alishinda Kombe la Dunia la Vilabu na Ligi ya Conference na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wakati alipokuwa Stamford Bridge, ashawahi kufanya kazi na City.

    Alikuwa msaidizi wa Guardiola wakati Man City iliposhinda mataji matatu 2022-23 na alishikilia jukumu muhimu katika chuo cha mafunzo ya soka ya ya klabu hiyo kabla ya kujiunga na kikosi cha kwanza.

    Guardiola aliwahi kumsifia Maresca kama: "Mmoja wa makocha bora duniani. Ninamfahamu vyema Maresca, lakini kazi aliyoifanya Chelsea haijapewa uzito unaostahili.''

    Soma pia:

  4. Ebola huenda inaenea kwa kasi zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali, daktari wa WHO aonya

    Mlipuko huo ulioanzia DR Congo, pia umeenea hadi nchi jirani ya Uganda

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mlipuko huo ulioanzia DR Congo, pia umeenea hadi nchi jirani ya Uganda

    Mlipuko wa Ebola ambao umesababisha vifo vya takriban watu 131 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda ukaenea kwa kasi zaidi kuliko ilivyodhaniwa awali, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameonya.

    Dkt Anne Ancia aliiambia BBC kwamba kadiri shirika hilo linavyochunguza ndivyo inavyodhihirika kuwa maambukizi yameenea katika maeneo mengine.

    Maafisa walisema zaidi ya watu 513 wanashukiwa kuambukizwa nchini DR Congo kufikia Jumanne, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki katika nchi jirani ya Uganda.

    Utafiti wa Kituo cha MRC chenye makao yake mjini London cha Uchambuzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Ulimwenguni uliotolewa Jumatatu ulipendekeza kulikuwa na "ugunduzi mkubwa" wa chini, na kwamba haiwezi kudhibiti kuwa tayari kulikuwa na kesi zaidi ya 1,000.

    Utafiti huo ulipendekeza kuwa mlipuko wa sasa ni "mkubwa kuliko ilivyothibitishwa sasa" na kwamba "uhalisia wa ukubwa wake bado haujabainika".

    Shirika la Msalaba Mwekundu lilionya kwamba Ebola inaweza kusambaa haraka ikiwa walioambukizwa hawatatambuliwa mapema, kwa sababu jamii hazina habari na mifumo ya afya imezidiwa, na kuongeza kuwa "tunashuhudia haya yote" katika mlipuko wa sasa.

    Siku ya Jumatatu Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi alitoa wito wa "utulivu" na kuwataka raia wa Congo kuwa makini na kuzingatia ushauri wa wahudumu wa afya, baada ya kufanya mkutano wa dharura na maafisa wake Jumatatu jioni.

    Mkuu WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye alitangaza mlipuko huo kuwa janga la kimataifa wiki iliyopita, alisema "ana hofia sana na ukubwa na kasi ya janga hilo".

    Pia unaweza kusoma:

  5. Mgomo wa wahudumu wa usafiri wa umma wasitishwa Kenya

    .

    Wahudumu wa usafiri wa umma nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa nchi nzima baada ya mazungumzo na serikali kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta.

    Wahudumu hao wanasema wamesitisha mgomo huo kwa siku 7 hadi Jumanne wiki ijayo ili kutoa fursa ya mazungumzo zaidi na serikali.

    Makubaliano ya kusitisha mgomo huo yalitangazwa Jumanne na Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen kufuatia mashauriano ya dharura yaliyolenga kukomesha adha kwa maelfu ya wasafiri waliokwama Nairobi na miji mingine mikuu.

    "Mgomo umesitishwa kwa muda wa wiki moja ili kutoa mwanya wa mashauriano na mazungumzo kati ya serikali na washikadau," Murkomen alisema.

    Mgomo huo ulichochewa na ongezeko kubwa la bei ya mafuta iliyotangazwa wiki iliyopita, huku wahudumu wa uchukuzi wakionya kuwa kupanda kwa gharama ya dizeli kumevuruga shughuli zao.

    Maandamano hayo pia yalizua machafuko katika baadhi ya maeneo ya nchi, baada ya polisi kukabiliana vikali na waandamanaji walioweka vizuizi vya barabarani, kusababisha usumbufu mkubwa.

    Watu wanne waliuawa katika maandamano hayo na wengine thelathini kujeruhiwa.

    Jumatatu jioni, serikali ilitangaza kupunguzwa kwa bei ya dizeli kwa shilingi kumi kwa lita kama sehemu ya kutuliza mvutano.

    Bei ya mafuta taa iliongeza kwa shilingi 38 kwa lita.

    Awali wahudumu wa usafiriwa umma walikuwa wameshinikiza kupunguzwa kwa bei ya mafuta ya dizeli kwa shilingi 46 lakini baadaye walikubali kusitisha mgomo huo kwa muda ili kutoa nafasi kwa mazungumzo zaidi.

    Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Edwin Mukabane, mwenyekiti wa kitaifa wa Shirikisho la Sekta ya Usafiri wa Umma, alionya kwamba wahudumu wa sekta hiyo watarejekea tena mgomo ikiwa matokeo ya mazungumzo hayo hayatkuwa na tija.

    "Tunapisha mazungumzo ... lakini tunawaarifu wateja na wale tunaofanya nao kazi kuelewa kwamba ikiwa suala hili haitatatuliwa ndani ya siku saba tulizokubaliana, mgomo utarejea," alisema.

  6. Je, Arsenal kutwaa ubingwa wa EPL leo?

      • Author, Abdalla Seif Dzungu
    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kocha Mikel Arteta wa Arsenal akimkumbatia Saka

    Arsenal inakaribia kushinda taji la kwanza la Ligi ya Premia ndani ya miaka 22 kwa kupata ushindi mnono wa 1-0 dhidi ya Burnley hapo jana katika mchezo wake wa mwisho nyumbani, kupitia bao lililofungwa na Kai Havertz kipindi cha kwanza.

    Matokeo hayo yanamaanisha Manchester City wanaoshika nafasi ya pili lazima wasitishe rekodi ya Bournemouth ya kutopoteza mechi 16 hii leo ili kupeleka pambano la kuwania taji hilo hadi wikendi ya mwisho.

    Matumaini ya Manchester City ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza yanategemea kushinda mechi zao zilizosalia na kutumaini Arsenal itapoteza pointi.

    Kwa sababu The Gunners wanaongoza kwa pointi nyingi kukiwa na mchezo mmoja pekee, City lazima washinde Bournemouth na Aston Villa huku Arsenal wakipoteza au wapate sare dhidi ya Crystal Palace.

    Hata hivyo, Arsenal itatawazwa bingwa ikiwa itaifunga Crystal Palace ugenini siku ya Jumatatu.

    Litakuwa ni taji la kwanza la ligi kwa Arsenal tangu 2004, wakati "Invincibles" ilipocheza msimu wote bila kushindwa hata mechi moja chini ya meneja wa wakati huo Arsene Wenger.

    Meneja wa sasa Mikel Arteta atalazimika kushinda mechi mbili zilizosalia ili kuipatia timu yake msimu bora zaidi kuwahi kutokea katika klabu hiyo kwani Arsenal pia inacheza na Paris Saint-Germain kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mnamo Mei 30.

    Soma pia:

  7. Zaidi ya waandamanaji 710 wakamatwa nchini Kenya

    Lango kuu la ofisi za upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Lango kuu la ofisi za upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya

    Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya, imetangaza kuwa imewakamata Zaidi ya watu 710 kufuatia maandamano yaliyofanyika nchini humo siku ya Jumatatu, kupinga kupanda kwa bei ya mafuta.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa na idara hiyo, wale watakaopatikana wakitenda uhalifu kipindi hiki cha maandamano watachukuliwa hatua kali za kisheria.

    “Kila mkenya ana haki ya kikatiba ya kukongamana na kutoa maoni yao kwa amani, vitendo vya vurugu, uporaji, kuchoma mali, kuziba barabara, kuharibu miundombinu, kushambulia polisi au madereva, na vitendo vyovyote vinavyohatarisha maisha ni makosa makubwa ya jinai,” idara hiyo ilisema kupitia ukurasa wao wa X.

    Kulingana na DCI, uchunguzi kuhusu maandamano hayo bado unaendelea, huku zaidi ya watu 710 wakikamatwa katika maeneo tofauti nchini Kenya.

    Watu 259 walikamatwa eneo la bonde la ufa, watu 189 walikamatwa mjini Nairobi, watu 142 walikamatwa eneo la kati mwa Kenya, watu 103 Mashariki mwa Kenya, huku watu 10 wakikamatwa Magharibi na Pwani mwa taifa hilo

    “Washukiwa tayari wamefikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka mbalimbali,” DCI imesema.

    Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta nchini Kenya yameingia siku yake ya pili hii leo.

  8. Meli za wanaharakati zilizokuwa zimebeba misaada kuelekea Gaza zimezuiliwa na Israel

    Wanajeshi wa Israel kwenye msafara wa Flotilla

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel kwenye msafara wa Flotilla

    Wanaharakati wanaowaunga mkono Wapalestina wanasema vikosi vya Israel vimezuia msafara wao wa meli zaidi ya 50 zilizokuwa zikibeba misaada kuelekea eneo la Gaza katika maji ya kimataifa magharibi mwa Cyprus.

    Msafara wa Global Sumud (GSF) umesema meli zake ziliingiwa kwa nguvu katika kile walichokiita “shambulio haramu la baharini” umbali wa takriban kilomita 460 (km kutoka Gaza. Video za moja kwa moja zilionyesha wanajeshi wa Israel wakipanda baadhi ya meli hizo.

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema operesheni hiyo “inalenga kuzuia mpango mbaya uliolenga kuvunja kizuizi cha kijeshi tulioweka dhidi ya magaidi wa Hamas huko Gaza.”

    Mwezi uliopita, vikosi vya Israel pia vilizuia meli 22 kutoka kwa msafara huo karibu na kisiwa cha Krete, wanaharakati 181 waliokuwa ndani ya meli hizo walizuiliwa, na wote isipokuwa wawili waliachiliwa huru katika kisiwa hicho cha Ugiriki.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Inspekta wa Polisi Kenya akamatwa kwa kuwaachilia washukiwa wa maandamano

    Picha ya zamani ya polisi wakiwakamata waandamanaji nchini Kenya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya zamani ya polisi wakiwakamata waandamanaji nchini Kenya

    Mkuu wa kituo cha Polisi cha Central jijini Nairobi, Dishen Angoya anaripotiwa kukamatwa asubuhi Jumanne kufuatia kuachiliwa huru kwa washukiwa waliokamatwa kutokana na maandanamo ya jana ya kupinga kwa bei ya mafuta ambayo yalisababisha vifo vya watu wanne.

    Kulingana na ripoti za Mei 19, mamlaka iliamuru kukamatwa kwa Inspekta Dishen baada ya watu waliokuwa wamezuiliwa kwa makosa ya kusababisha vurugu kwa umma, kuachiliwa kutoka kizuizini.

    Katika kitabu rasmi cha matukio kinachotumiwa katika kituo cha polisi kurekodi kila tukio kwenye kituo cha polisi cha Central, rekodi ya tukio hilo imesema.

    "Inspekta Mkuu wa Polisi Dishen Angoya, OCS wa kituo kuu cha polisi cha Central, eneo la Nairobi amekamatwa na Naibu Kamanda wa polisi kwa kosa la kutumia vibaya ofisi, jana 18/05/2026 alitumia mamlaka vibaya na kuwaachia washukiwa sitini na nne(64) waliokuwa wamekamatwa kwa makosa yanayohusiana na kusababisha vurugu. Kwa sasa amewekwa katika kituo cha polisi akisubiri hatua zaidi kuchuliwa huku akilalamikia shinikizo la juu la damu," taarifa hiyo inasema.

    Uchunguzi wa tukio hilo umeanza.

    Soma zaidi:

  10. Barabara zasalia tupu nchini Kenya, siku ya pili ya maandamano yakupinga kupanda kwa bei ya mafuta

    Barabara ya Waiyaki Way, mjini Nairobi
    Maelezo ya picha, Barabara ya Waiyaki Way, mjini Nairobi

    Usafiri wa umma nchini Kenya umeathirika kwa siku ya pili, mgomo wa kitaifa wa magari ya uchukuzi ukiendelea.

    Barabara nyingi nchini Kenya, haswa mji wa Nairobi, zimesalia tupu, huku wasafiri kadhaa wakionekana kutembea kwa miguu kutokana na ukosefu wa magari.

    Barabara zilivyosalia tupu mjini Nairobi kwa picha:

    Picha ya barabara kuu ya Express Way
    Maelezo ya picha, Picha ya barabara kuu ya Express Way
    Baadhi ya watu wakitembea kutokana na ukosefu wa magari
    Maelezo ya picha, Baadhi ya watu wakitembea kutokana na ukosefu wa magari
    Picha ya barabara ya Express Way
    Maelezo ya picha, Picha ya barabara ya Express Way
  11. Marekani yaondoa vikwazo dhidi ya mafuta ya Urusi kwa mara ya pili

    Picha ya mafuta ikiwekwa kwa gari

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya mafuta ikiwekwa kwa gari

    Marekani imetangaza kuongeza muda wa kuondolewa vikwazo kwa mafuta ya Urusi yaliyoko baharini kwa siku 30, ili kuzisaidia mataifa yaliyo katika hatari ya kukosa mafuta.

    Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, alisema “tumetoa leseni ya muda kusaidia mataifa yaliyoko kwenye hatari zaidi kununua mafuta ya Urusi, na leseni hii itasaidia kuimarisha bei ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa” Kiongozi huyo alichapisha kwenye mtandao wa X.

    Bessent, ambaye awali alisema kuwa hakukuwa na mpango wa kuongeza tena msamaha huo wa vikwazo vya mafuta ya Urusi, alidai kuwa hatua hiyo itasaidia kuhakikisha mataifa yenye uhitaji, yanapata mafuta.

    Hii ni mara ya pili kwa wizara ya fedha ya Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya mafuta ya Urusi.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Zaidi ya watu 3000 wamefariki nchini Lebanon kutokana na mashambulizi ya Israel

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza kuwa mashambulizi kati ya kundi la Hezbollah na Israel imesababisha vifo vya watu 3,020.

    Vita kati ya Hezbollah na Israel vilianza tena tarehe 2 mwezi Machi, baada ya kundi hilo kurusha makombora nchini Israel, baada ya kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei.

    Licha ya kuwepo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, idadi ya vifo kutokana na mashambulizi hayo imezidi kuongezeka, huku Lebanon na Israel wakiongeza muda wa kusitisha mashambulizi kwa siku 45, huku mazungumzo ya kupatikana kwa amani yakitarajiwa kurejelewa tena mapema mwezi Juni.

    Wizara ya Afya ya Lebanon imesema zaidi ya vifo 400 vimerekodiwa tangu kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano ulioafikiwa tarehe 17, mwezi Aprili.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Masomo, biashara zaendelea kuathirika siku ya pili ya mgomo wa usafiri wa umma

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Shule kadhaa zimeendelea kuahirisha masomo huku mgomo wa usafiri wa umma ukiingia siku ya pili.

    Hapo jana, kuna shule ambazo zilituma ujumbe mapema kujulisha wazazi kutowapeleka watoto wao shuleni huku waliofika, wakilazimika kuondoka mapema na wazazi kutumiwa ujumbe wa kufuata watoto kwa hofu ya usalama wao.

    Hali ni vivyo hivyo kwa wafabiashara wa jijini Nairobi ambako maeneo mengi bado yamesalia kufungwa na barabara zikiwa zimesalia mahame.

    Taarifa iliyotolewa Jumapili ya kuanza kwa mgomo huo, ilijumuisha usafiri wa abiria, mizigo na vifaa, huduma za usafiri, usafiri wa pikipiki, usafiri wa utalii, shule za udereva, mabasi ya shule na madereva binafsi.

    Sekta ya wahudumu wa usafiri wa umma ilisema kuwa washikadau wote wameamua kuungana ili kukabiliana na kile walichokiita kupanda kwa bei ya mafuta na mazingira magumu ya uchumi wakisisitiza kuwa hilo linaongeza gharama ya usafiri, chakula, umeme na bidhaa muhimu kwa mahitaji ya binadamu.

    "Hatua hii sio tu kwa wahudumu wa usafiri wa umma, lakini kwa kila raia wa Kenya. Mwananchi wa kawaida ndiye mwathirika mkuu wa bei ya juu ya mafuta,"muungano huo ulisema.

    Pia unaweza kusoma:

  14. Watu 131 wafariki kutokana na Ebola nchini DRC

    Picha ya mhudumu wa afya akimulekekeza mgonjwa kunawa mikono

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya mhudumu wa afya akimulekekeza mgonjwa kunawa mikono

    Takriban watu 131 wameripotiwa kufariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku zaidi ya visa 513 vikiripotiwa, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Msemaji wa serikali ya DRC ametangaza kuwa visa vya ugonjwa huo kwa sasa vinaripotiwa kutoka maeneo tofauti nchini humo ikilinganishwa na awali.

    Mkurugenzi wa CDC barani Afrika, Jean Kaseya ameonya kuwa hakuna dawa ya kutibu aina hii ya Ebola, na umakini unafaa kuzingatiwa pakubwa na wahudumu wa afya na wakati wa mazishi ya walioathirika na ugonjwa huu.

    Visa viwili vya ugonjwa huu vimeripotiwa nchini Uganda, na kisa kimoja cha kifo.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa janga la kimataifa.

    Pia unaweza kusoma:

  15. Hakuna makubaliano yaliyofikiwa na wahudumu wa usafiri wa umma Kenya

    .

    Mkwamo kati ya serikali na washikadau katika sekta ya usafiri wa umma ulikuwa bado haujatatuliwa kufikia Jumatatu usiku baada ya mazungumzo yaliochukua saa kadhaa kushindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mgomo ambao umeathiri usafiri wa umma kote nchini.

    Mazungumzo yaliyoongozwa na Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir na Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi yaliendelea hadi jioni, lakini hadi wakati pande hizo mbili zinazungumza na vyombo vya habari, hakuna makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa yapata saa tatu na nusu usiku.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, Wandayi awali alipendekeza kwamba hatua imepigwa na kwamba majadiliano yamekuwa yenye tija. Hata hivyo, maafisa kutoka sekta ya matatu walikatiza mkutano huo, wakisisitiza kwamba hakuna makubaliano ya mwisho yaliyofikiwa.

    Baadaye usiku, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (EPRA) ilitoa taarifa ikisema imepunguza bei ya deseli kwa shilingi 10 huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa shilingi 36 na kupunguza tofauti kubwa ya bei iliyokuwepo.

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Soma zaidi:

  16. Bei ya diseli yashuka huku wahudumu wa usafiri wa umma wakiapa kuendelea na mgomo Kenya

    Mafuta

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli nchini Kenya (EPRA) imepunguza bei ya diseli baada ya mgomo wa usafiri wa umma uliokuwa unapinga kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo hapo jana, 18/05/2026 na kutatiza shughuli mbalimbali kote nchini Kenya.

    Kwa sasa bei ya mafuta imeshuka kwa shilingi 10 huku bei ya mafuta taa ikipanda kwa shilingi 38 ilhali bei ya petroli ikisalia jinsi ilivyo.

    Bei hizi mpya zinaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 19/05/2026 hadi 14/06/2026.

    Taarifa hii imetolewa baada ya wahudumu wa sekta ya umma kulalamika kuwa tofauti kubwa iliyopo kati ya diseli na mafuta taa inahatarisha uwezekano wa uchakachuaji na ulaghai katika upatikanaji wa mafuta safi.

    Wahudumu wa matatu wameapa kuendelea na mgomo wao hii leo kwa siku ya pili baada ya mkutano wao na serikali kushindwa kufikia makubaliano.

    Wameendelea kushikilia kuwa mgomo wa kupinga kupanda kwa bei za mafuta utaendelea hadi kilio chao kitakaposikilizwa.

    Soma zaidi:

  17. Trump atangaza kusitisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran, akidai karibu wanaafikia makubaliano

    Picha ya Donald Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya Donald Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kuwa ameagiza kusitishwa kwa shambulio jipya la kijeshi dhidi ya Iran kwa ombi la viongozi wa mataifa ya Kiarabu ya eneo hilo, akiongezea kuwa mazungumzo na Tehran karibu yanaafikia makubaliano ambayo yataizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.

    Trump alisema kuwa amesitisha operesheni za kijeshi kwa siku mbili au tatu ili kutoa nafasi kwa mazungumzo hayo kufanyika pamoja na mashauriano na viongozi wa eneo kutoka Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Qatar.

    Iran pamoja na mataifa hayo ya Kiarabu hazijajibu matamshi ya Trump, lakini makao makuu ya jeshi la Iran mjini Tehran yalisema vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo “vina nguvu zaidi na vimejiandaa zaidi kuliko hapo awali.”

    Pia unaweza kusoma:

  18. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Jumanne ya leo