Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini mabango yenye maneno 'sio eneo la kupigana busu' yanawekwa huko Mumbai?
Huko Mumbai, unaweza kuwa umeona maneno 'HAKUNA KUVUTA SIGARA HAPA'' au 'HAKUNA KUPAKI GARI' au 'HAKUNA KUTEMA' barabarani, kwenye bustani au katika ofisi za serikali.
Lakini katika jamii moja eneo la Borivali kumeandikwa 'HILI SI ENEO LA KUPIGANA BUSU' barabarani mbele ya jengo moja.
Jamii ya Satyam-Shivam Sundaram iliamua kuandika maneno 'Hakuna Kupigana Busu Hapa' kwani walikuwa wamechoshwa na utani mchafu unaofanywa na wenza wapenzi wanapokuwa barabarani.
Kulingana na jamii, hii iliandikwa kutokana na mapendekezo ya wenyeji.
Kwanini sio eneo la kupigana busu?
Jamii ya Satyam-Shivam Sundaram iliandika maneno 'Hakuna Kupigana Busu Eneo Hili' miezi miwili iliyopita.
Lakini yote hayo yalianza kipindi cha kutakiwa kusalia ndani.
Wakaazi wa jamii wanasema kwamba magari yalianza kuegeshwa katika barabara ya eneo hilo kipindi cha kutakiwa kusalia ndani..
Baada ya hapo, wavulana na wasichana wakawa wanakuja katika barabara hiyo kupunga upepo.
Lakini, polepole kwenye baiskeli, kwenye magari, wenzi hawa wanaopendana walianza utani.
Kisha ikageuka na kuwa utani mbaya.
Utani huu mchafu wa wapenzi ulionekana kwanza na Ruchi Parekh, ambaye anaishi katika jengo hilo.
Akizungumza na BBC, anasema "Wakati wa kutotoka nje, wapenzi walikuwa wanakuja asubuhi na jioni. Lakini, walikuwa wakifanya mizaha michafu zaidi kuliko kubusu. Tulijaribu kuzungumza nao ili kuwashawishi kuacha, na baada ya hapo, wakaazi walipiga picha na kuchukua video za wenzi hao wakiwa wamekaa barabarani wakifanya mizaha michafu na kesi hiyo ikaenda kwa polisi.
Vinay Ansunkar, rais wa jamii hiyo, anasema, "Polisi walikuwa wanakuja na kuwafukuza wapenzi hao".
Lakini baada ya polisi kuondoka, wavulana na wasichana hao walikuwa wakirudi tena.
"Kwa hivyo, kama onyo kwa wenzi wapenzi, jamii iliamua kuandika 'HILI SI ENEO LA KUPIGANA BUSU' katika barabara hiyo mnamo mwezi Mei.
Lakini hili wazo la 'HILI SI ENEO LA KUPIGANA BUSU' lilitokea wapi?
Wazo hilo lilipendekezwa kwa Vinay Ansunkar, Rais wa jamii ya eneo, anasema, "Tunaona mabango mengi ya aina hiyo huko Mumbai.
Watu wengi katika jamii walikuwa wakiulizia cha kufanya kuzuia ngono ya watoto.
Wakazi wa jamii wanasema kwamba hakuna chochote kibaya kwa wavulana na wasichana kusimama hapa na kupiga soga.
Lakini, vitendo vya kushawishi watoto kuingia kwenye ngono vinapaswa kuachwa.
Ruchi anaendelea kusema, "Sio tu kuhusu kupigana busu. Ni juu ya kufanya mizaha michafu. Utani wa aibu wa wavulana na wasichana hawa hauwezi kusemwa kwa maneno".
'Tulikuwa tukifunga madirisha'
Kulingana na wakaazi wa jamii hiyo, wenzi hao walikuja na kukaa hapa karibu saa kumi na moja jioni.
Ruchi Parekh anaendelea kusema, "Wakati wa jioni tulikuwa tukikusanyika pamoja kunywa chai au kupiga soga. Lakini, kwasababu ya utani huu mbaya wa watoto, tulilazimika kuhakikisha madirisha yanafungwa. Kuna watoto na watu wazima ndani ya nyumba. Na haiwezekani kwao kuona kinachoendelea".
Wakazi wanasema majaribio kadhaa yalifanywa kuwashawishi wavulana na wasichana.
Waliwashawishi, wakati mwingine wao wenyewe na wakati mwingine kwa kumtuma mlinzi.
Je! Ulifaidika kwa kuandika 'HAKUNA KUPIGANA BUSU ENEO HILI'
Ruchi anasema, baada ya kuandika 'HAKUNA KUPIGANA BUSU' ENEO HILI', sasa wavulana na wasichana wameacha kuja.
Wakati mwingine wavulana na wasichana huja, lakini sasa utani huu mchafu hawaufanyi tena mbele ya jamii yetu.
"Sipingi kupigana busu. Lakini watu hukasirika sana na utani huu mchafu", Vinay Ansunkar aliongeza.
Lakini mapenzi ni nini hasa. Watoto wanahitaji kuelewa hili, anasema.