Shangwe, vifijo, nderemo zilisheheni miji mbalimbali watu wakisherehekea kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2019 katika majiji mbalimbali duniani, fataki nazo zikatanda angani.
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Fataki hapa zinaonekana London Eye ambapo zilirushwa angani kwa dakika 10 hivi katikati mwa London
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, "Yellow Vest", waandamanaji wanaovalia fulana za rangi ya manjano nchini Ufaransa walikuwa miongoni mwa waliokuwa wanaandamana karibu na Champs-Elysees jijini Paris
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Hapa, fataki zinaonekana juu ya sanamu ya Quadriga katika lango maarufu la Brandenburg Gate, Berlin
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Wanandoa hawa nao wanaonekana wakikoleza upendo wao kama sehemu ya sherehe za kuulaki Mwaka Mpya eneo la Red Square, Moscow
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Jijini Nairobi, fataki zinaonekana zikirushwa angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Na hapa, mwanaulimbwende anaonekana akipamba nywele ya mmoja wa watu waliojitokeza mjini Ahmedabad, India kwa sherehe za kuulaki mwaka mpya
Chanzo cha picha, AFP/Getty
Maelezo ya picha, Maelfu walikusanyika pia Pyongyang, Korea Kaskazini kwa maonesho ya fataki katika uwanja wa Kim Il Sung
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Hapa ni fataki zikirushwa na watu ufukweni Gangneung, katika mkoa wa Ganwon, Korea Kusini
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, Dubai, fataki zilikuwa tele pia
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Ufilipino, huyu aliamua kuvalia miwani ya 'kumsaidia kuuona vyema' Mwaka 2019 katika sherehe iliyofanyika katika eneo la Metro Manila, jijini Quezon
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Waumini wa Kibuddha nao hapa wanaonekana wakiwasha mishumaa kuukaribisha Mwaka wa Nguruwe kwa mujibu ya miaka ya nyota ya Kichina katika hekalu la Jogyesa jijini Seoul, Korea Kusini
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Hapa watu wanaonekana wakijaribu kupiga picha fataki zilizorushwa kwenye jengo refu maarufu la Taipei 101 nchini Taiwan
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Anga ya Hong Kong pia ilipambwa kwa fataki watu wakiukaribisha mwaka 2019 nchini China
Chanzo cha picha, Lintao Zhang/Getty Images
Maelezo ya picha, Sherehe ya Mwaka Mpya pia ilifanyika Beijing, China
Chanzo cha picha, AFP/Getty
Maelezo ya picha, Na Marina Bay, Singapore kulikuwepo uhondo zaidi
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Huko Sydney Harbour Bridge nchini Australia, maonyesho ya fataki yalidumu dakika 12