Tazama: Dakika za mwisho kabla ya Marekani kukamata meli ya Iran
Tazama: Dakika za mwisho kabla ya Marekani kukamata meli ya Iran
Vikosi vya Marekani vimeikamata meli ya mizigo yenye bendera ya Iran katika Ghuba kama sehemu ya kizuizi chake cha majini, Donald Trump amesema.
Rais wa Marekani aliandika kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba Touska ilikamatwa na Jeshi la Wanamaji la Marekani baada ya kukaidi amri ya kutia nanga.
Iran imetaja hatua hiyo kama ukiukaji wa usitishaji mapigano na kuapa kulipiza kisasi hivi karibuni "kitendo hicho cha uharamia".
Centcom (Kamandi Kuu ya Marekani) imetoa video mbili ambazo zimeunganishwa katika uhariri huu.
Wanasema video moja inaonyesha meli ya Iran ikionywa kabla ya risasi kurushwa. Ya pili, wanasema, inaonyesha Wanajeshi wa majini wa Marekani wakiondoka kwenye meli yao na kupanda meli ya Iran.



