Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Arsenal na Chelsea zamfukuzia Lewis Hall

Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal na Chelsea wanaongoza katika harakati za kumsajili Lewis Hall, 21 wa Newcastle, lakini timu hiyo hawatamruhusu beki huyo wa kushoto kuondoka kirahisi. (Caught Offside)

Liverpool na Manchester United wanamtaka nahodha wa RB Leipzig, David Raum baada ya kuvutiwa na beki huyo wa kushoto wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 27 wakati wa ziara ya kusaka wachezaji msimu huu. (Teamtalk)

Bart Verbruggen wa Brighton huenda akaondoka Seagulls msimu huu wa joto huku kipa huyo wa Uholanzi, 23, akifikiria chaguzi mbalimbali kuhusu mustakabali wake. (Florian Plettenberg)

Chelsea ingependa kumsajili winga wa Porto, Mbrazili William Gomes, 20, kwenye safu yao ya ushambuliaji kwa msimu ujao. ( Sport Witness)

Liverpool wanatarajiwa kumpa mkataba mpya kipa wao raia wa Brazil, Alisson Becker mwenye umri wa miaka 33 msimu ujao. (Football Insider)

Kiungo wa zamani wa Liverpool na Paris St-Germain Georginio Wijnaldum ana hamu ya kurejea Ligi Kuu England msimu ujao, huku mkataba wa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 35 na klabu ya Saudi Arabia Al-Ettifaq ukikamilika msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Swansea wameweka bei ya pauni milioni 15 kwa mshambuliaji wa Slovenia Zan Vipotnik, 24, ambaye anaongoza chati ya wafungaji mabao katika michuano ya Championship na Brighton wanamtaka. Football Insider)

Real Madrid itasikiliza ofa za kumuuza mshambuliaji wa Uhispania, Gonzalo Garcia, 22, msimu huu wa joto lakini itakataa nia yoyote ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 19 Endrick, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Lyon. (The Athletic)

Juventus itajaribu kumuuza mshambuliaji Lois Openda, 26, baada ya kulazimika kumsajili Mbelgiji huyo msimu huu wa joto mwishoni mwa mkopo wake kutoka RB Leipzig. (Fabrizio Romano)