Fahamu hatua tatu za mapendekezo ya Iran ya kusitisha mapigano

Chanzo cha picha, Tasnim
Mtandao wa Lebanon Al-Mayadeen unasema Iran imeeleza kuwa mazungumzo yanaweza kuanza tena ikiwa Marekani itakubali pendekezo lake.
Mwandishi wa Al-Mayadeen aliyeko Tehran aliandika katika ripoti kwamba pendekezo la Iran lina "hatua tatu": kumaliza vita, kusimamia Mlango wa Bahari wa Hormuz, kisha mazungumzo kuhusu nyuklia.
Maafisa wa Marekani na Iran bado hawajatoa maoni rasmi. Ikulu ya Marekani (White House) imesema inachambua "ujumbe ulioandikwa" kutoka Tehran. Baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vinasema kwamba Donald Trump hafurahishwi sana na pendekezo la Iran.
Mtandao wa Lebanon wa Al-Mayadeen una uhusiano wa karibu na Iran na Hezbollah.
Kulingana na Al-Mayadeen, Iran inataka Marekani na Israel kwanza wamalize vita vinavyoendelea Iran na Lebanon, na kutoa dhamana kwamba hakutakuwa na mashambulizi tena dhidi ya nchi hizi mbili.
Baada ya hatua ya kwanza, mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mlango wa Bahari wa Hormuz yataanza kwa uratibu na Oman ili kuandaa mfumo wa kisheria wa utawala na usafiri katika njia hii ya maji.
Baada ya kukamilika kwa hatua ya kwanza na ya pili, Iran na Marekani zinaweza kuanza mazungumzo kuhusu masuala ya nyuklia.
Kulingana na ripoti hii, Iran haitashiriki katika suala la nyuklia hadi hatua mbili za kwanza zitakapokamilika.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, alisafiri kwenda Muscat na Islamabad mara mbili katika siku chache zilizopita, kisha akakutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Saint Petersburg.
Wakati huo huo, viongozi wa nchi za Ghuba ya Uajemi wanashiriki katika mkutano wa dharura wa Baraza la nchi za Ghuba huko Jeddah, ambao ni mkutano wa kwanza wa baraza hilo tangu kuanza kwa vita na Iran.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa wa kikanda ambaye hakutaka kutajwa jina akisema kuwa mkutano huo unalenga kuandaa majibu dhidi ya maelfu ya mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran.
Vita hivyo vimeharibu miundombinu muhimu ya nishati katika nchi zote sita wanachama, na pia kampuni zinazohusishwa na Marekani zimelengwa, pamoja na baadhi ya miundombinu ya kiraia na vituo vya kijeshi.
Mazungumzo kati ya Marekani na Iran ya kufikia makubaliano ya kudumu na kumaliza vita hadi sasa hayajazaa matunda, na nchi za Ghuba ya Uajemi zina wasiwasi kuhusu athari zake.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Gulf Cooperation Council inakabiliwa na ukosoaji kutoka United Arab Emirates kwa majibu yake yasiyoridhisha kuhusu vita.
Anwar Gargash, mshauri mwandamizi wa serikali ya UAE, alisema:
"Ni kweli kwamba nchi za GCC zilitoa msaada wa vifaa (lojistiki), lakini kisiasa na kijeshi, kwa maoni yangu, msimamo wao umekuwa dhaifu zaidi katika historia."
"Nilitarajia msimamo dhaifu kama huo kutoka Umoja wa nchi za KiarabuArab sishangai, lakini sikutarajia kutoka Baraza la Ushirikiano (GCC) na nimeshangazwa."














