Tetesi za Soka Ijumaa: Arsenal bado wamng'ang'ania Alvarez

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Zikisalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa rasmi, Arsenal hawajakata tamaa katika harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 26, ambaye inadaiwa anataka kuondoka Atletico Madrid. (Mail).
Manchester City wanamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Everton Iliman Ndiaye, 26, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 80. (Guardian)
Aston Villa imewasiliana moja kwa moja na AC Milan kuhusu winga wa Ureno Rafael Leao, 27, katika jitihada za kuipiku Galatasaray katika mbio za kumsajili. (Fabrizio Romano)
Nottingham Forest imewasilisha ofa yenye thamani ya hadi pauni milioni 22 kwa beki wa pembeni wa Crystal Palace na Colombia, Daniel Munoz, 30. (Athletic)
Atletico Madrid inafikira kuwasajili washambuliaji wa Brazil Igor Jesus, 25, wa Nottingham Forest na Gabriel Jesus, 29, wa Arsenal. (Fichajes)
Napoli inataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Newcastle na Ujerumani Nick Woltemade, 24. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa Chelsea na Argentina Enzo Fernandez, 25, bado ana matumaini ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester City. (Fabrizio Romano)
Manchester United wamepewa fursa ya kumsajili beki wa kati wa Chelsea, Tosin Adarabioyo, 28, huku timu hiyo chini ya Michael Carrick ikitafuta kuimarisha safu yake ya ulinzi. (GiveMeSport)
Hull City wako karibu kufikia makubaliano na AS Roma kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Robinio Vaz, 19. (Athletic)
Chelsea wako katika mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji wa Hiispania Marc Guiu, 20, kwenda Napoli. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Fiorentina na Italia Moise Kean anazidi kukaribia kujiunga na Como katika uhamisho unaoweza kufikia takriban pauni milioni 35. (Sky Sports Italy)
Leeds United wamemruhusu kipa wa Brazil Lucas Perri, 28, kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Torino, kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja. (Sky Sports)
Wakati huohuo, Leeds United wanafikiria kumsajili kipa wa Standard Liege na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC, Matthieu Epolo, 21. (Get French Football News)














