Viumbe wanaoishi maisha marefu na mafupi zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa uhai wa mwanadamu unachukua takriban miongo minane, kwa upande mwingine kuna viumbe ambao huishi kwa mami ya miaka, na wengine huishi kwa saa chache tu kabla ya kufariki.
Swali la kwanini kuna tofauti hii ya umri wa kuishi kati ya viumbe, jibu liko katika utenda kazi wa mwili, mazingira, na uzazi.
Ikiwa spishi inakabiliwa na uwindawaji au mabadiliko makali ya misimu, kuwekeza nishati katika kurekebisha seli huwa ni kupoteza muda, spishi hizi huwa na ukuaji wa haraka, uzazi wa mapema, na maisha mafupi.
Katika maji baridi na yenye kina kirefu yenye oksijeni kidogo na viumbe wanaowinda viumbe wengine ni wachache, kupunguza kasi ya metaboliki ili kupunguza uharibifu wa seli na mwili kutochoka mapema, hufanya viumbe hawa kuwa na muda wa kutosha wa kurekebisha DNA, na kuwezesha maisha marefu sana.
Viumbe wa maisha marefu
Wakati wa kupima uzeekaji miongoni mwa viumbe, ikolojia ya baharini inatoa fursa nzuri zaidi. Halijoto ya baridi na kupungua kwa kasi ya metaboliki, huruhusu viumbe wa baharini kuwa na maisha marefu kwa karne nyingi.
Yavuyavu (Immortal Jellyfish)

Chanzo cha picha, gettyimages
Yavuyavu asiyezeeka ama kwa kitaalamu Turritopsis dohrnii, ndio kiumbe cha ajabu zaidi Duniani, Yavuyavu asiyezeeka huepuka kifo cha asili kupitia mchakato unaoitwa transdifferentiation.
Anapokabiliwa na tatizo katika mazingira, uharibifu wa kimwili, au njaa, Yavuyavu hafi. Badala yake, huirudisha ndani minyiri yake, hurudi kwenye seli changa, na kutulia kwenye sakafu ya bahari ili kuanzisha upya mzunguko wake wa maisha.
Yavuyavu anaweza kurudia mzunguko huu bila kikomo, na hilo humpa uwezo wa kutokufa kibiolojia isipokuwa aliwe au afe kwa ugonjwa.
Sifongo za glasi (Hexactinellida)

Chanzo cha picha, National Oceanic and Atmospheric Administration (NOAA).
Katika kina kirefu cha baharini huko Antaktika viumbe ambao kitaalamu huitwa Hexactinellida ama kwa Kiengereza Ocean Quahogs, wanakadiriwa kuishi hadi miaka 10,000, wakiishi katika maji ya baridi sana.
Hwa ni viumbe kutoka jamii ya konokono wanaoishi muda mrefu. Sampuli inayoitwa "Ming," iliyokusanywa pwani ya Iceland, ilibainishwa kuwa ganda lake kuwa na umri wa miaka 507 lilipovuliwa mwaka 2006.
Papa wa Greenland (Somniosus microcephalus)

Chanzo cha picha, Getty Images
Miongoni mwa wanyama wenye uti wa mgongo, papa wa Greenland ndio huishi maisha marefu. Wakiwa wanakaa kwenye kina cha barafu cha Atlantiki Kaskazini, wanyama hawa wanaowinda polepole hukua chini ya sentimita moja kwa mwaka.
Wanabiolojia wa baharini waligundua kwamba papa wa Greenland hawafikii hata balehe hadi wafikie umri wa miaka 150. Papa mzee zaidi aliyepimwa alikadiriwa kuwa na umri wa takriban 392.
Papa hawa walikuwa wakiogelea katika maji ya Aktiki wakati Isaac Newton akiwa hai.
Viumbe wa maisha mafupi
Katika upande mwingine wa viumbe vinavyoishi muda mfupi. Viumbe hivi, huzeeka haraka hadi kiwango ambapo uhai wa kiumbe mzee humruhusu kufanya jambo moja tu.
Kipepeo aina ya Mayfly (Ephemeroptera)

Chanzo cha picha, gettyimages
Jina la Ephemeroptera linatokana na neno la Kigiriki ephemeros , linalomaanisha "siku moja.” Jina linalofaa kwa kiumbe mwenye umri mfupi zaidi wa kuishi duniani.
Ingawa kipepeo aina ya mayf hutumia mwaka mmoja hadi miwili kuishi ndani ya maji kama buu (nymph), hatua yao ya mwisho ya utu uzima huchukua kati ya dakika 30 na saa 24, kulingana na spishi.
Vipepeo aina ya mayf waliokomaa hawana sehemu za mdomo au njia za kumeng'enya chakula zinazofanya kazi; hawawezi kula. Awamu yao yote ya utu uzima ipo tu kwa ajili ya kujamiiana, kutaga mayai, na kufa.
Minyo aina ya Gastrotrichs

Chanzo cha picha, GFDL o
Minyoo aina ya Gastrotrichs ni wanyama wadogo, kama minyoo wanaopatikana katika mazingira ya maji safi na baharini. Maisha yao yote kuanzia yai hadi ukubwa yanadumu kwa takriban siku 3 hadi 10.
Wakati wa kipindi hiki cha muda mfupi, hula mwani na bakteria, huzaa mayai, na hukamilisha mzunguko wao wa maisha kabla ya uharibifu wa seli kuanza.
Kinyonga aina ya Labord (Furcifer labordi)

Chanzo cha picha, iNaturali
Miongoni mwa wanyama wenye uti wa mgongo wa nchi kavu, ni kinyonga Labord wa Madagasca, ambaye anashikilia rekodi ya maisha mafupi zaidi.
Hutambaa na huishi kwa jumla ya miezi 4 hadi 5, ambayo karibu yote hukaa ndani ya yai. Huanguliwa mwanzoni mwa msimu wa mvua mwezi Novemba.
Kisha hukua haraka hadi kukomaa katika wiki chache tu, hujamiiana, hutaga mayai yao, na hufa ifikapo Aprilina kuacha spishi hiyo ikiishi kama mayai yaliyozikwa wakati wa msimu mrefu wa kiangazi.















