Moja kwa moja, Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema katika saa 48 zilizopita vikosi vya Iran vilifanyia majaribio kwa mara ya kwanza kombora lililotengenezwa nchini humo dhidi ya meli ya Marekani.

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Mbappé ajitosa katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, amesema anaamini anaweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.

    Mbappé, mwenye umri wa miaka 27, amefunga mabao 42 katika mechi 44 akiwa na Real Madrid msimu huu, licha ya kutoshinda taji lolote akiwa na klabu hiyo.

    Katika Kombe la Dunia, Mbappé alifunga mabao 10 na kutwaa Kiatu cha Dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo.

    Mbappé pia alivunja rekodi ya ufungaji mabao katika historia ya Kombe la Dunia, akifikisha jumla ya mabao 22. Ufaransa ilimaliza katika nafasi ya nne baada ya kushindwa kufuzu kwa fainali.

    Akizungumzia nafasi yake ya kushinda Ballon d’Or, Mbappé amesema jina lake limekuwa likitajwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo.

    “Labda mwaka huu ni mwaka mzuri kwangu kushinda tuzo hiyo, lakini wapiga kura huangalia kiwango cha uchezaji,” Mbappé aliwaambia waandishi wa habari.

    Nyota huyo wa Ufaransa hajawahi kushinda Ballon d’Or. Nafasi yake ya juu zaidi ilikuwa ya tatu mwaka 2023.

    Miongoni mwa wachezaji wengine wanaotajwa kuwa na nafasi ya kushinda tuzo hiyo mwaka huu ni Harry Kane, Lamine Yamal na Rodri.

  2. IRGC yatishia meli zinazotumia njia ya kusini ya Hormuz

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Naibu Mkuu wa Siasa wa Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, IRGC, amesema eneo la Khasab nchini Oman ndilo mwisho wa njia salama kwa meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

    Khasab ni mji ulioko katika ncha ya kaskazini ya Oman, karibu na Mlango wa Hormuz.

    Vyombo vya habari vya Iran vimemnukuu Ali Mohammadi akisema kupita kwa usalama katika njia ya kusini ya Mlango wa Hormuz, inayodhibitiwa na Marekani, kwa sasa ni jambo lisilowezekana.

    Amesema meli yoyote itakayotumia njia hiyo haitakuwa tena salama dhidi ya hatari ya kushambuliwa itakapofika katika eneo la Khasab.

    Taarifa za meli kushambuliwa karibu na Khasab zilianza kutolewa mwanzoni mwa vita vya siku 40, huku matukio hayo yakiongezeka katika siku 10 zilizopita.

    Hata hivyo, bado haijafahamika ni nani anayehusika na mashambulizi hayo, na hakuna upande uliodai rasmi kuhusika.

    Naibu Mkuu huyo wa Jeshi la Wanamaji la IRGC amezitaka meli zote zinazopita katika Mlango wa Hormuz kutumia njia iliyo upande wa Iran.

    Amesema IRGC itafuatilia kwa karibu mienendo ya meli katika Ghuba ya Uajemi, Mlango wa Hormuz na Ghuba ya Oman, kwa kutumia uwezo wake wa kijasusi na kijeshi.

    Ameongeza kuwa jeshi hilo litaendelea kufuatilia mienendo ya meli katika maeneo hayo.

  3. Tetesi za Soka Jumanne: Chiesa kuondoka Liverpool

    f

    Chanzo cha picha, PA Media

    Mshambuliaji wa Liverpool, Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 26, huenda akaondoka klabuni hapo Januari iwapo atakosa muda wa kutosha wa kucheza baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha.. (Football Insider), external

    Winga wa zamani wa Manchester United, Jadon Sancho, yuko kwenye mazungumzo na angalau klabu mbili za Ligi Kuu ya England kuhusu uwezekano wa kujiunga nazo.(Teamtalk)

    AC Milan inapanga kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Brazil, Endrick, mwenye umri wa miaka 20, kutoka Real Madrid mwezi Januari. (Calciomercato, external)

    Manchester United bado inamtaka kiungo wa Leicester City, Louis Page, mwenye umri wa miaka 18, baada ya kushindwa kumsajili siku ya mwisho ya dirisha la usajili. (ESPN, external)

    Manchester City inaendelea kumfuatilia kiungo wa Atletico Madrid, Alex Baena, mwenye umri wa miaka 25, ingawa huenda klabu hiyo isifanye uhamisho wake Januari. (Football Insider)

    Liverpool na Manchester United zimewasiliana moja kwa moja na Wolves kuhusu uwezekano wa kumsajili winga mwenye umri wa miaka 18, Matheus Mane.(Ekrem Konur}

    Brentford imeanza mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wake Mjerumani, Kevin Schade, mwenye umri wa miaka 24, katika jitihada za kuzuia Arsenal kumnasa.(Teamtalk)

    Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 16, Isaac Konde.(Fabrizio Romano)

    Soma Pia:

  4. Iran yasema ina uwezo wa kuzishambulia meli za kivita za Marekani

    e

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran, Majid Ibn e Reza, amesema jeshi la Iran lina uwezo kamili wa kushambulia meli za kivita za Marekani zinazotekeleza kizuizi cha majini dhidi ya Iran.

    Kauli hiyo inakuja baada ya maafisa wa Iran kudai kuwa vikosi vyao vilishambulia meli mbili za kivita za Marekani katika Ghuba ya Uajemi kwa kutumia silaha za kushambulia meli.

    Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema katika saa 48 zilizopita vikosi vya Iran vilifanyia majaribio kwa mara ya kwanza kombora lililotengenezwa nchini humo dhidi ya meli ya Marekani. Hata hivyo, wataalamu wanasema aina ya kombora lililotumika haijathibitishwa kwa uhuru.

    Kwa upande mwingine, Kamandi Kuu ya Marekani, CENTCOM, haijajibu moja kwa moja madai hayo.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema ikiwa Iran itashambulia meli mbili za Marekani, Marekani itasababisha madhara makubwa zaidi na kuharibu meli tatu za Iran.

    CENTCOM pia imesema haitasita kulinda vikosi vya Marekani na, ikibidi, kuharibu meli za Iran.

    Soma pia:

  5. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.