Moja kwa moja, Mbunge wa Marekani: Trump na washirika wake wamenufaika na vita dhidi ya Iran

Hakuna ushahidi unaothibitisha moja kwa moja madai ya Warren kuhusu uhusiano kati ya michango ya kampeni na faida zinazodaiwa kupatikana kutokana na vita hivyo.

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Tishio dhidi ya mwana wa Netanyahu lasababisha kuondolewa kwake MarekanI

    Netanyahu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Vyombo kadhaa vya habari vya Israel vimeripoti kuwa shirika la usalama wa ndani la nchi hiyo, Shin Bet, limethibitisha kile lilichokitaja kuwa tishio kubwa dhidi ya Yair Netanyahu, mwana wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

    Kwa mujibu wa ripoti hizo, tathmini ya usalama ilisababisha uamuzi wa kumhamisha Yair Netanyahu kutoka Marekani kwenda Israel pamoja na kikosi chake cha ulinzi.

    Taarifa hizo zimekuja baada ya kuibuka kwa ripoti kuhusu safari yake ya dharura kutoka Florida kwenda Israel. Shin Bet haijatoa maelezo zaidi kuhusu asili ya tishio lililoripotiwa au waliotuhumiwa kuhusika.

    Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu alidai kuwa Iran ilikuwa imejaribu kumuua mmoja wa wanawe, ingawa hakumtaja kwa jina wakati huo. Ripoti za sasa zinaeleza kuwa alikuwa akimuashiria Yair Netanyahu.

    Kwa upande wake, Iran imewahi kukanusha madai ya kuhusika katika njama za mauaji dhidi ya viongozi au watu mashuhuri wa kisiasa wa Marekani na Israel. Kufikia sasa, Tehran haijatoa tamko rasmi kuhusu taarifa mpya zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Israel.

    Maelezo zaidi:

  2. Mbunge wa Marekani: Trump na washirika wake wamenufaika na vita dhidi ya Iran

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

    Seneta wa chama cha Democratic, Elizabeth Warren, amemtaja Donald Trump kuwa "rais fisadi zaidi katika historia ya Marekani" wakati akimkosoa kuhusu sera zake kuhusiana na Iran na sekta ya mafuta.

    Akizungumza katika mkutano wa kampeni, Warren alidai kuwa baadhi ya makampuni makubwa ya mafuta yaliyounga mkono kampeni ya Trump yamenufaika pakubwa kutokana na vita dhidi ya Iran.

    "Donald Trump anapoanzisha vita na Iran na marafiki zake wa sekta ya mafuta, ambao walichangia kampeni yake, wakipata faida kubwa kutokana na vita hivi, ni wajibu wetu kufichua hali hiyo na kuipinga," alisema Warren.

    Warren hakutaja kampuni yoyote mahsusi kuhusiana na madai hayo. Wakati huo huo, ongezeko la bei ya mafuta na faida kubwa zilizoripotiwa katika baadhi ya kampuni za sekta ya nishati limekuwa likifuatiliwa kwa karibu na wachambuzi katika miezi ya hivi karibuni.

    Hata hivyo, hakuna ushahidi uliowasilishwa unaothibitisha moja kwa moja madai ya Warren kuhusu uhusiano kati ya michango ya kampeni na faida zinazodaiwa kupatikana kutokana na vita hivyo.

    Kwa upande wake, Trump amewahi kukosoa kupanda kwa bei ya mafuta na kuwataka wazalishaji kuongeza uzalishaji ili kusaidia kudhibiti bei.

    Soama zaidi:

  3. Natumai hujambo. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.