Moja kwa moja , Iran yasema haiwezi kuzuiwa kwa vikwazo vya ardhini huku Marekani ikiongeza vikwazo vya kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Abbas Araqchi, amesema kuwa, kuizuia Iran kupitia vikwazo vya ardhini ni jambo ambalo haliwezekani kutokana na ukubwa wa nchi hiyo.

Muhtasari

Iran yasema haiwezi kuzuiwa kirahisi kwa vikwazo vya ardhini

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Iran yasema haiwezi kuzuiwa kwa vikwazo vya ardhini

    .
    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Abbas Araqchi

    Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Abbas Araqchi, amesema kuwa, kuizuia Iran kupitia vikwazo vya ardhini ni jambo ambalo haliwezekani kutokana na ukubwa wa nchi hiyo, pamoja na uhusiano na miingiliano iliyopo kati ya majimbo yake, miji na jamii zinazoishi katika maeneo ya mpakani.

    “Kuizuia Iran kupitia vikwazo vya ardhini ni jambo ambalo karibu haliwezekani, kutokana na ukubwa wa nchi yetu na idadi kubwa ya majimbo, ambayo kila moja lina uwezo na rasilimali tofauti. Majimbo hayo yana uhusiano mpana na majimbo jirani katika nchi zinazopakana na Iran, ikiwemo shughuli nyingi za usafiri, uhusiano wa kijamii kati ya wananchi pamoja na mizizi ya kihistoria na kitamaduni inayowaunganisha watu wa pande zote za mipaka,” alisema Araqchi.

    Aidha, Waziri huyo wa Mambo ya Kigeni alisema kuwa kwa maoni yake, Tehran inapaswa kuendelea na diplomasia itakayosaidia kupunguza vikwazo vinavyoikabili taifa hilo.

    “Njia bora ya kukabiliana na shinikizo hizi ni kuhakikisha kuwa vikwazo havifikii malengo yake, ili wanaoviweka watambue kuwa njia hiyo haifanyi kazi na haitafanya kazi.”

    Kulingana na kiongozi huyo, wanaitaka Iran iwe na uwezo wa kustahimili vikwazo vyote,ili kuiwekea Iran vikwazo isiwe na maana tena.

    “Hakuna ambaye anafaa kufikiria kuwa anaweza kuilazimisha Iran kujisalimisha kwa kuongeza shinikizo la kiuchumi na vikwazo.”

    Soma pia:

  2. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja Jumanne ya leo