Ni nani anayelinda meli eneo la Ghuba na Bahari ya Shamu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya Iran kuendelea kuudhibiti Mlango Bahari wa Homuz, kama hatua ya kulipiza kisasi mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi yake mnamo Februari 28, Uingereza na Ufaransa zimekuwa zikiongoza juhudi za usalama baharini kulinda biashara za kimataifa katika ukanda huo muhimu ambapo asilimia 20 ya mafuta duniani husafirishwa.
Hivi majuzi Uingereza na Ufaransa, pamoja na nchi nyingine 24, zilitangaza kuunga mkono kuanzishwa kwa ujumbe "huru wa kujihami" wa jeshi la kimataifa ili kuondoa mkwamo katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, wakati masharti yanayofaa yatakapotimizwa.
Nchi hizo 26 zilisema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza baada ya London na Paris kufanya mkutano wa mawaziri wa ulinzi na wawakilishi kutoka nchi 38 mnamo Mei 12 na kutangaza uungaji mkono wao kwa ujumbe huu, ambao unalenga kuzihakikishia usalama kampuni za biashara za meli na kutekeleza shughuli za kuondoa vilipuzi vya chini ya maji.
Je, ni miungano gani maarufu zaidi ya kijeshi kwa sasa inayolinda usafiri wa baharini katika eneo la Mashariki ya Kati?
Combined Task Force 153
Combined Task Force 153, ambayo kwa sasa inaongozwa na Misri, ilianzishwa Aprili 17, 2022. Ni mojawapo ya vikosi vitano vya Jeshi la Wanamaji la Combined Marine Corps (muungano wa kimataifa wa kutoa ulinzi baharini), kufuatia matukio katika Bahari Shamu, hasa kurushwa kwa kombora kutoka eneo linalodhibitiwa na Houthis nchini Yemen.
Jukumu:
Kutoa ulinzi katika Bahari ya Shumu, Bab al-Mandab na Ghumba ya Aden, na kukabiliana na shughuli haramu, magendo na uharamia.
Mataifa muhimu yanayoshiriki:
Marekani, Ufaransa, Misri, Italia, na Australia.
Combined Task Force 153, inayoongozwa na Australia, ilipeleka meli nne zisizo na rubani kati ya Februari na Aprili 2026, zikishika doria katika eneo la shughuli zenye ukubwa wa kilomita za mraba 219,000, zinazofunika karibu nusu ya Bahari ya Shamu, kufuatilia shughuli zozote zisizo halali.
"Aspidis"
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tarehe iliyoanzishwa:
Kikosi cha wanamaji cha EU "ASPEDS" ni misheni ya baharini iliyotumwa katika Bahari ya Shamu. Ilianzishwa mnamo Februari 2024 kama operesheni ya kujihami ili kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara wapiganaji wa Kihouthi dhidi ya meli za kimataifa tangu Oktoba 2023, na mamlaka ya awali ambayo yanafanywa upya kila mwaka. Mamlaka yake yameongezwa hadi tarehe 28 Februari 2027.
Majadiliano yanaendelea ndani ya Umoja wa Ulaya kupanua majukumu ya Operesheni Aspidis kujumuisha Mlango-Bahari wa Hormuz.
Jukumu:
Kulinda meli na kuhakikisha uhuru wa urambazaji katika Bahari ya Shamu, Ghuba ya Aden, Bahari ya Arabia, Bahari ya Oman, Ghuba, na Kaskazini Magharibi mwa Bahari ya Hindi.
Makao makuu: Ugiriki
Nchi muhimu zinazoshiriki: Ufaransa Ujerumani, Italia na Ubelgiji
Mnamo Agost 2024, meli ya mafuta iliyo na bendera ya Ugiriki - MV Sounion, iliyokuwa imebeba tani 150,000 za mafuta ghafi, ilishambuliwa katika mastukio tofauti na watu waliokuwa wamejihami katika eneo la kusini mwa Bahari ya Shamu. Wafanyakazi wa meli hiyo waliomba usaidizi baada ya kushambuliwa.
Kujibu ombi hilo Aspidis ilituma chombo mahali hapo kukabiliana na na maharamia kuvamia meli hiyo ya mafuta, na wafanyikazi wote waliokolewa.
Combined Task Force "Sentinel"
Mnamo Julai 9, 2019, Mwenyekiti wa wakati huo wa Wakuu Jeshi la Marekani, Jenerali Joseph Dunford, alitangaza kuanzishwa kwa " Kuundwa kwa Muungano wa Kimataifa wa Usalama wa Baharini" ili kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka dhidi ya meli za kibiashara zinazovuka maji ya kimataifa katika eneo la Mashariki ya Kati. Miezi minne baadaye, Combined Task Force Sentinel, kitengo cha uendeshaji wa muungano huo, ulianzishwa.
Jukumu:
Meli kubwa za kivita kama vile frigates zina jukumu la kufuatilia vituo muhimu vilivyo na msongamano, wakati meli ndogo za kivita, kama vile boti za doria zinafuatilia njia za meli za doria. Ndege za upelelezi hufuatilia usafiri kupitia maeneo hatari zaidi. Eneo lao la uendeshaji ni pamoja na Mlango-Bahari wa Hormuz, Mlango-Bahari wa Bab el-Mandeb, Ghuba ya Oman, na Ghuba ya Uajemi.
Makao makuu: Bahrain
Nchi muhimu zinazoshiriki: Muungano huo unajumuisha nchi tisa wanachama: Albania, Bahrain, Estonia, Lithuania, Romania, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uingereza na Marekani.
Operesheni ya "Atlanta"
Mwishoni mwa 2008, Umoja wa Ulaya ulianzisha Operesheni Atalanta ili kuzuia uharamia na wizi wa kutumia silaha katika pwani ya Somalia. Misheni hiyo iliongezewa muda wa kuhudumu mnamo Desemba 2024 hadi Februari 2027, na mamlaka mpya inajumuisha maeneo mengine kama Ghuba ya Aden na nchi jirani, ikiwa ni pamoja na jiji la bandari la Muscat, Bahari ya Shamu, Ghuba ya Suez na Ghuba ya Aqaba.
Jukumu:
Kutoa ulinzi kwa meli za shilika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani zinazopeleka misaada ya chakula kwa watu waliofurushwa makwao nchini Somalia na meli zingine zinazokabiliwa na tishio la kushambuliwa na kuzuia vitendo vya uharamia na ujambazi wa kutumia silaha baharini.
Kikosi cha wanamaji cha Umoja wa Ulaya kinashika doria kwenye Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi.
Vyombo vya majini vya Umoja wa Ulaya vinatoa usaidizi kwa meli zinazokabiliwa na matatizo, ama kutokana na shambulio la maharamia au hali nyingine ya dharura baharini.
Makao makuu: Uhispania na Ufaransa.
Nchi kuu zinazoshiriki:
Norway, Ukraine, New Zealand, Serbia, na Montenegro.
Mnamo tarehe 29 Novemba, ujumbe wa "Atalanta" ulitangaza kwamba vikosi vyake "vilifanikiwa kutoa msaada kwa meli ya Yemeni ambayo ilipata hitilafu kubwa ya mitambo na iliripotiwa kupotea katika maji mashariki mwa Ghuba ya Aden."














