Fahamu faida za kiafya za kula miguu ya kuku

.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 4

Umewahi kufikiria jinsi kula miguu ya kuku kunaweza kukupatia faidaza kiafya?

Baadhi ya watu wanadhani wanadhani kuwa miguu ya kuku haina faida, lakini huko Singapore, miguu ya kuku huuzwa kwa dola nne za Singapore kwa kilo.

Ni ghali zaidi kuliko nyama ya kuku katika nchi kama Afrika Kusini na Mexico.

Miguu ya kuku ina mahitaji makubwa duniani kote. Nchi kama vile Vietnam, China, na Uzbekistan huagiza kiasi kikubwa cha miguu ya kuku ili kukidhi mahitaji yao ya chakula. Mnamo 2022, Marekani ilisafirisha takriban tani 133,000 za miguu ya kuku kwenda Uchina.

Ni nini kinachofanya miguu ya kuku, ambayo huchukuliwa kuwa taka na kutupwa, kuwa na thamani kubwa katika sehemu nyingine za dunia?

Virutubisho vinavyopatikana kwenye miguu ya kuku

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ingawa miguu ya kuku inachukuliwa kuwa taka katika baadhi ya nchi, kulingana na utafiti iliyochapishwa na Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani (NIH), ina virutubishi vingi muhimu na faida za kiafya.

Marekani inaendesha biashara kubwa zaidi ya kuku wa nyama duniani, huku takriban asilimia 15 ya uzalishaji wake ukiuzwa nje ya nchi nyingine. Hii inajumuisha sehemu kubwa ya miguu ya kuku.

Mwanasoka maarufu wa Uingereza, Andros Townsend, aliwahi kuiambia BBC: "Miguu ya kuku ina nyama kidogo, lakini ni tamu zaidi kuliko kuku wengine. Wanaliwa kwa hamu kubwa katika nchi kama vile Uchina, Afrika Kusini na Ureno, na wanaweza kupikwa kwa dakika 20 tu."

Miguu ya kuku imeundwa na ngozi, mifupa, misuli, na tishu zinazounganishwa. Kulingana na utafiti, muundo wao una karibu asilimia 30 hadi 35 ya collagen.

Miguu ya kuku ina kalori nyingi, protini, mafuta, wanga, na pia virutubishi kama kalsiamu, vitamini A, na vitamini B9.

Mtaalamu wa lishe ya afya wa Chennai, Dk. Sri Vidya, anaelezea kuwa karibu 70% ya jumla ya protini katika miguu ya kuku ni collagen.

Collagen ni protini ambayo pia iko katika mwili wa binadamu. Inapatikana katika ngozi, mifupa, tendons, cartilage, na mishipa inayounganisha viungo.

Kulingana na karatasi ya utafiti iliyochapishwa na Taasisi za Kitaifa za Afya za Merika (NIH), miguu ya kuku ina virutubisho vingi muhimu na faida za kiafya.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini kadri mwili unavyozeeka, uzalishaji wa asili wa collagen hupungua.

Dkt Srividya anasema kuwa mwili wa binadamu unafyonza kwa urahisi collagen inayopatikana katika miguu ya kuku. Collagen ina jukumu muhimu katika afya ya ngozi na mifupa.

Alieleza kuwa kadri tunavyozeeka, mwili hutoa collagen kidogo, ambayo husababisha ngozi kuwa kavu na mikunjo. Hii pia huathiri afya ya viungo na mifupa.

Kulingana na Dkt. Srividya, collagen na gelatin katika miguu ya kuku ina manufaa kwa afya kwa ngozi, viungo, mifupa na utumbo. Mapitio ya tafiti kwa wagonjwa wenye ugonjwa wa yabisi iligundua kuwa kula collagen hupunguza kukakamaa kwa viungo.

Aliongeza kuwa "protini, vitamini, na madini inayopatikana kwenye miguu ya kuku pia husaidia katika ukuaji wa misuli na nywele."

Inafaa kuliwa vipi?

.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Dr. Srividya anasema ni muhimu kuosha vyema miguu ya kuku kabla ya kuanza kuandaa mapishi. Anaonya kuwa miguu ya kuku isiposafishwa vizuri inaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya bakteria.

Pia aliongeza ni muhimu kuondoa ngozi ya nje na kupika hadi iive vizuri. Miguu ya kuku ambayo haijaiva vizuri inaweza kuwa na bakteria kama vile salmonella na campylobacter.

Profesa Ono Suparno wa Chuo Kikuu cha IPB aliandika katika makala ya afya kwamba miguu ya kuku ni bora kuliko aina nyingine ya supu, kama vile miguu ya mbuzi.

Dk Srividya alisema hii ni kwa sababu collagen na gelatin kwenye miguu ya kuku ni bora zaidi na inastahili kupikwa vyema ili mwili uweze kufyonza kwa urahisi. Wanaweza pia kufanywa kwa supu nyepesi au mchuzi, lakini kukaanga kunapaswa kuepukwa.

Alionya kuwa miguu ya kuku wa kukaanga inaweza kuwa na madhara kwa afya. Wana mafuta mengi, mafuta na sodiamu, ambayo ni hatari kwa moyo.

Nani anaweza kula na kwa kiwango gani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Dr. Srividya anasema vitamin B9 inayopatikana kwenye miguu ya kuku ina manufaa ya kiafya kwa wanawake wajawazito, lakini anasisitiza umuhimu kuitumia kwa kiasi kinachofaa.

Aliongeza kuwa kila mtu anaweza kula gramu 100 hadi 150 za miguu ya kuku iliyopikwa na kutengenezwa supu au mchuzi.

Kulingana naye, wakati wa kuwapa watoto, wanapaswa kufundishwa kuitafuna vizuri kabla ya kumeza. Haiwezi kutolewa kwa watoto ambao bado hawana meno, wala kwa watu wazima ambao hawana meno au ambao wana shida kumeza.

Alionya kuwa "chakula hiki kinaweza kukwama kwenye koo na kusababisha hatari ya kiafya. Ikumbukwe pia kwamba kina mafuta mengi."