Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nini kinasababisha nywele kupotea?
Ikiwa wewe ni mwanamme au mwanamke, kupoteza nywele linaonekana ni tatizo la watu wengi. Suala hili huathiri hisia za mtu na kisha athari hii ya kihisia inageuka kuwa tatizo kubwa katika maisha.
Kulingana na utafiti uliofanywa nchini India, karibu 50% ya wanaume na 40% ya wanawake wanaofikia umri wa miaka 50 wanakabiliwa na tatizo la kupoteza nywele. Kwa wastani, nywele 80 hadi 100 huanguka kati ya nywele milioni 100 hadi 150 kila siku.
Kupoteza nywele kuko kwa aina mbili. Zile zinazopote na kutorudi tena. Na zile zinazopotea na kisha zinaweza kurudi.
Sababu za nywele kupotea
Kuna sababu nyingi za kupoteza nywele, ambazo zinahusiana na maisha ya kila mtu. Pia kupoteza nywele kunaweza kusababishwa na sababu za msimu. Sababu za kibinafsi zinaweza kujumuisha vinasaba, au sababu zinazohusiana na afya.
Baadhi ya sababu za upotezaji wa nywele ziko nje ya uwezo wetu na muundo wa jeni ndio sababu kuu.
Pia, sababu ya homoni ambayo ni ya kawaida kwa wanaume na nadra kwa wanawake. Wanawake wengi hupoteza nywele baada ya kujifungua kutokana na kutofautiana kwa homoni. Kupoteza nywele kwa wanawake kunaweza kusababishwa na mabadiliko ya asili ya homoni.
Pia, upotezaji wa nywele unaweza kusababishwa na kula dawa au magonjwa fulani. Mfano matibabu kwa mionzi wakati wa matibabu ya saratani.
Kinga dhaifu inaweza pia kuwa sababu nyingine ya kupoteza nywele, ambayo inaweza kudhibitiwa tu na matibabu ya kawaida.
Baadhi ya magonjwa ya fangasi au matatizo kama vile mba ni tatizo lingine kwa nywele. Msongo wa mawazo ni sababu nyingine ambayo inaweza kusababisha kupoteza nywele.
Namna ya Kujikinga
Wataalamu wamependekeza baadhi ya hatua za kuchukua ili kuwa na ukuaji mzuri wa nywele. Sugua kichwa chako na mafuta ya uvuguvugu ya nazi angalau mara mbili kwa wiki na kisha osha nywele zako.
Usitumie kitambaa kila wakati kukausha nywele zako. Funika kichwa chako wakati wa hali mbaya ya hewa na vumbi ili nywele zako zisikauke. Usiache nywele zako wazi kila wakati. Kutumia kemikali mara kwa mara kunaweza kusababisha nywele kupukutika.
Nywele nyeusi, ndefu na nzuri huchukuliwa kama ishara ya urembo na uzuri, lakini ikiwa nywele zako hazifikii viwango hivi, badala ya kuwa na wasiwasi, furahiya namna ulivyo.